PREZO AMWITA DIAMOND MWAJUMA SOMA ALICHOKIPOST HAPA

starlisha_full1 Starlisha Tillya aka Chagga Barbie au The First Lady aliekuwa mpenzi wa prezo

Wakati huu unaweza kuwa wakati wa kucheka kiaina kwa Huddah Monroe ambaye kwa kipindi kirefu alinyimwa raha na tambo za mrembo wa kitanzania aishie Marekani, Starlisha Tillya aka Chagga Barbie au The First Lady ambaye alikuwa analimiliki penzi la mfalme wa bling bling Jackson Makini aka Prezzo.

Prezzoprezo
Hali imebadilika sasa na inaonesha dhahiri Starlisha na Prezzo wamepigana chini, na hasira zimemsababisha mrembo huyo amechukua uamuzi wa kupost kwenye mitandao ya kijamii baadhi ya message za Prezzo alizochart naye zinazomponda mkali wa Bongo Fleva, Diamond Platinumz.
“Kufanya nyimbo na Davido kalipa $3000 wala davido hajam acknowledge kabisa.” Inasomeka message ya Prezzo, “Kiingereza Shida huh” inasomeka message nyingine, huku mrembo huyo akionesha kushangaa, “Mbona nasikia Davido kamualika!.”
Starlisha amemponda Prezzo na kumwagia maatusi katika post kadhaa na kudai kuwa mkali huyo wa ‘Lighter’ humuita Diamond Mwajuma.

chagga-2Mesage za Starlisha Tillya  na prezo zikimponda Diamond

diamondDiamond Platnum

Unatengeneza ma video yasiyo na kiwango Kutwa kumponda Diamond Mara ngapi nimemtetea huyu kinara wa East Africa usiyemkubali wewe unamuita mwenzio sijui Mwajuma wewe na yeye Nani Mwajuma kaa sio wewe. Natafuta namba ya kuweka ur voice notes watu wakusikilize kibuyu wewe.” Yanasomeka maandishi haya kwenye post nyingine iliyomalizika kwa matusi ya makali ya nguoni.
Chagga Barbie amedai kuwa Prezzo amekuwa akimbembeleza amuwish birthday kwa kumpost kwenye mitandao ili aonekane, lakini pia kumuomba ticket na kuomba mrembo huyo amnunulie Sneakers.
Mwaka jana Prezzo aliingia katika beef na Diamond Platinumz kutokana na maandishi ya gazeti moja la Kibongo, lakini Prezzo alimuomba msamaha Diamond aliyetaka aombwe msamaha huo kupitia mitandao ya kijamii kama alivyomponda kupitia mitandao hiyo. Kitu ambacho Prezzo alikiita ‘Utoto’.
Hata hivyo beef hilo liliyeyuka.

Usisahau kulike and share pia unatupata facebook .  swahili movies .com
pia follow us instagram  swahilimovies

Habari kwa msaada wa clouds

KAJALA AANZISHA KAMPUNI YAKE YA FILAMU “KAY ENTERTAINMENT”, LAANA NI FILAMU YAKE YA KWANZA KUITENGENEZA.

 

1kajala21kajala

Baada ya kipindi kirefu sasa kupita bila Kajala Masanja kuonekana kwenye filamu za kampuni ya Wema Sepetu(Endless Fame Productions)  iliyodaiwa kumsainisha na kampuni hiyo kudaiwa kuyumba kwa kukosa
usimamizi mzuri sasa muigizaji huyo aliyejaaliwa mvuto amekuja kivingine mwenyewe mwaka huu kwa kuanzisha kampuni yake ya movies na issue nyingine za productions. Habari za uhakika ni kuwa Kampuni ya kajala inaitwa “Kay Entertainment” na tayari muigizaji huyo anashuti filamu yake mpya ya kwanza kama producer na muigizaji kupitia kampuni hiyo. Filamu hiyo inaitwa “Laana” na director ni Leah Mwendamseke(Lamata). Ukiachilia mbali Kajala waigizaji wengine wa filamu hiyo ni pamoja na Gabo, Farida Sabu(Mama Sonia) na wengineo na hizo hapo chini ni baadhi ya picha za utengenezaji wa movie hiyo……………..

IMG-20140115-WA0004kajala na wasanii wakipitia script

IMG-20140115-WA0005Lamata, Gabo, Kajala na Farida Sabu(Mama Sonia) wakiwa on set

Usisahau kulike and share pia unatupata facebook .  swahili movies .com
pia follow us instagram  swahilimovies

Habari na picha kwa msaada wa swahili world planet blogsport