V.a.d film production ya Denmark kufungua Matawi ulimwengu mzima

10485878_10204076935954334_1016782931_n

Hi kuusu mipango mpya ya v.a.d film production. kutokana na wa pendwa na wa shabiki kupenda kupata kazi za V.A.D FILM PRODUCTION kwa haraka. tuna mpango kutokana na kikao tuliofanya juzi hivyo , sehemu yoyote duniani kukiwa mtu anaye penda kufanya kazi na V.A.D tutatoa vitumbali mbali zenye nembo za V.A.D GROUP na kufungua moja kwa moja mlango wa kazi zetu karibu na wa shabiki wetu kuanzia mwaka kesho .

tutakua na toa picha za vituo vyetu sehemu yeyote DUNIANI na adresse kwa kupata vitu vyetu…  pia watu wote wanaotaka kufanya kzi na VAD popote duniani waweze kuwasilina na VAD kw anuani ambazo zipo kwenye Adress za picha hapo juu au hapo chini .Apo kuna picha ya kikao ya viongozi wa V.A.D FILM PRODUCTION, na picha za vitambulisho tutatoa kwa sehemu tutakao fungua kazi zetu. na sehemu izo watu watapata DVD..

10499776_10204076947914633_453228657_o

10477621_10204076934674302_1619088223_n                             bango la Vad likiwa na picha za waigizaji wake10482718_10204076940914458_407684861_o

Viongozi na wasanii wa V.a.d wakiwa kwenye kikao

photokl
vitambulisho vya Vad
Follow us on instagram swahili movies and Like our facebook pages Swahili movies.com and  for more updates about Swahili movies latest news, Scandal, Celebrities, features,european news, American,Australian ,Africa news, Music , news and more

CREDIT : here

Tupe maoni yako hapo Chini..!!

Wema Azimia, Aunty Ezekiel Ampepea Kwa Dakika 29, Kajala Atajwa.

Capture.PNGma

Chuki tu! Katika jambo ambalo limeuumiza moyo wa Miss Tanzania 2006/07, Wema  Sepetu tangu awe star, ni ishu iliyotokea wikiendi iliyopita baada ya mtu asiyejulikana kutengeneza picha chafu ya mama mzazi wa mrembo huyo, Mariam Sepetu na kisha kuisambaza kwenye mitandao ya kijamii kitu ambacho kilimshtusha na kujikuta akipoteza fahamu/kuzimia

Akizungumza na Globalpublishers mmoja wa marafiki zake wa karibu ambaye aliomba chondechonde asitajwe jin lake alisema kwamba, mara ya mwisho kuona chozi la Wema ni siku ya msiba wa marehemu baba yake, mzee Sepetu lakini hili lilizidi kilio kile kwani ni tukio la udhalilishaji kwa mzazi wake huyo hivyo kuzimia ilikuwa ni lazima kwani yaliyomkuta yanasikitisha.

wemasepetu (1)

wema sepetu

Chanzo hicho kilidai kwamba, Wema hakutegemea kama ipo siku mama yake atadhalilishwa kiasi hicho hadi kufikia yeye kupoteza fahamu.

“Kiukweli ile picha ilichafua sana hali ya hewa hasa kwa wanaompenda Wema na hata kwa wanaomchukia Wema kwani kila mmoja alikuwa analaani kitendo kile ambacho si cha kiungwana.
“Unajua inafika hatua unatakiwa ufahamu mama wa mwenzio ni mama yako pia halafu usifurahie ubaya anaofanyiwa mama wa mwenzio tutukanane sisi wenyewe na si kuwaingiza wazazi kwenye mambo wasiyojua mbele wala nyuma,” kilidai chanzo hicho.
“Hebu fikiria mama yako mzazi atengenezewe picha ya utupu na jamii iaminishwe kuwa ni yeye wakati si kweli, inauma sana jamani. Utadhani huyo mtu hajazaliwa na mama.”
TIMU DENGUE NA MKAKATI MZITO
Katika kipindi cha vuguvugu la kuchafuana kilichoanza mwanzoni mwa wiki iliyopita, kuna wachangiaji katika mitandao ya kijamii waliojiita kwa jina la Timu Dengue, walionekana kumkandia Wema.

aunty

Chanzo hicho kinadai kuwa, timu hiyo ina mkakati mzito wa kumchafua Wema kwa kila namna.
“Wamepanga mkakati mzito, wanadai eti Wema anajisikia. Lakini watu wanasema haiwezekani watu wafanye mambo bila sababu. Sasa hapo wanamhusisha Kajala (Masanja) kwa kuwa ndiye mtu aliye na bifu naye kwa sasa,” kilipasha chanzo hicho na kuongeza:
“Lakini kuna wengine wanabishana, wanadai kuwa inawezekana watu wasio na kazi za kufanya au wenye chuki binafsi na Wema wameamua kutumia mwanya huo kumchafua Wema na familia yake wakiamini lazima Kajala atahusishwa kwa kuwa ana ugomvi naye.”
Globalpublishers iliposhuhudia picha hiyo ya utupu na kujiridhisha kuwa siyo ya mama Wema, lilimtafuta Wema kuzungumzia ni kwa jinsi gani alivyoumia baada ya kuona picha ile ambapo majibu yake alionekana bado ana maumivu makali ambayo yalidhihirisha wazi yalikuwa  hayajamuisha moyoni.
“Nimeumia sana mama yangu kudhalilishwa na si mimi tu familia yangu yote kwa jumla, tumeumizwa sana kwa tukio lile lakini mimi nasema namuachia Mungu kwani yeye ndiye anajua ila siyo siri ni tukio ambalo lilinifanya niugue ghafla,” alisema Wema na kuongeza:
“Yaani nilikuwa napewa pole nyingi sana utadhani mimi mgonjwa. Hata wale ambao hawanipendi nao walikuwa wakinipa pole. Naomba serikali itazame upya hili suala hili la watu kuchafuana kwenye mitandao ya kijamii.”
AUNT EZEKIEL AFANYA KAZI YA ZIADA
Katika ishu hiyo, staa mwenzake wa sinema Tanzania ambaye kwa sasa ni mashosti, Aunt Ezekiel alifanya kazi ya ziada kumuokoa Wema na kumfariji asichukue uamuzi mgumu.
Inaelezwa kuwa, Aunt alitumia dakika 29 kumpepea shosti wake huyo ili aweze kurejewa na fahamu, jambo zoezi ambalo lilizaa matunda.
Akizungumza na Globalpublishers kupitia gazeti la Risasi  Mchanganyiko, Aunty alisema tukio hilo limemuumiza kila mtu hata wale ambao wanaonekana wako tofauti na Wema lakini kwa hili nao wameumia na kuungana naye kumtetea na kuwakemea waliyofanya kitendo kile.

KIK

mamawema33

Wema na mama yake

“Nimeumia kwa tukio ambalo limefanywa na kusababisha Wema wangu kulia sana hadi kufikia kuumwa ghafla na kupoteza fahamu. Dah! Binadamu wengine sijui tukoje, lakini hamtaweza kufanikisha kwa sababu Wema ana watu wengi wanaompenda kuliko wanaomchukia,” alisema Aunt.
KAJALA SASA
Gazeti hili lilifanya jitihada za kumtafuta Kajala kupitia simu yake ya mkononi ili kujibu tuhuma za  kuhusishwa na picha hiyo lakini simu yake ilikuwa ikikatika kila ilipopigwa.
Baadaye ilijulikana kuwa, aliamua kuifunga kwa muda (inawezekana alikuwa sehemu inayohitaji utulivu).
Baadaye akatumiwa ujumbe uliosomeka: “Habari. Una taarifa ya picha chafu ya kutengenezwa ya mama Wema iliyosambazwa mitandaoni? Lakini unatajwa kuhusika kwa sababu una bifu na Wema, unasemaje?”
Hata hivyo mapaka gazeti linaenda mitamboni, Kajala hakujibu meseji hiyo wala kupiga simu chumba cha habari kufafanua kuhusiana na madai hayo ambayo bado hayajathibitishwa.
MAMA WEMA ANASEMAJE?
Jitihada za kuzungumza na mama Wema juu ya sakata hilo ziligonga mwamba kwani simu yake iliita bila kupokelewa.

FGG

kajala

kajala masanja

“Nimeumia kwa tukio ambalo limefanywa na kusababisha Wema wangu kulia sana hadi kufikia kuumwa ghafla na kupoteza fahamu. Dah! Binadamu wengine sijui tukoje, lakini hamtaweza kufanikisha kwa sababu Wema ana watu wengi wanaompenda kuliko wanaomchukia,” alisema Aunt.
KAJALA SASA
Gazeti hili lilifanya jitihada za kumtafuta Kajala kupitia simu yake ya mkononi ili kujibu tuhuma za  kuhusishwa na picha hiyo lakini simu yake ilikuwa ikikatika kila ilipopigwa.
Baadaye ilijulikana kuwa, aliamua kuifunga kwa muda (inawezekana alikuwa sehemu inayohitaji utulivu).
Baadaye akatumiwa ujumbe uliosomeka: “Habari. Una taarifa ya picha chafu ya kutengenezwa ya mama Wema iliyosambazwa mitandaoni? Lakini unatajwa kuhusika kwa sababu una bifu na Wema, unasemaje?”
Hata hivyo mapaka gazeti linaenda mitamboni, Kajala hakujibu meseji hiyo wala kupiga simu chumba cha habari kufafanua kuhusiana na madai hayo ambayo bado hayajathibitishwa.
MAMA WEMA ANASEMAJE?
Jitihada za kuzungumza na mama Wema juu ya sakata hilo ziligonga mwamba kwani simu yake iliita bila kupokelewa.
Follow us on instagram swahili movies and Like our facebook pages Swahili movies.com and  for more updates about Swahili movies latest news, Scandal, Celebrities, features,european news, American,Australian ,Africa news, Music , news and more

CREDIT : Swahiliworld palanet

Tupe maoni yako hapo Chini..!!