Tanzia: watanzania wote wanajulishwa juu ya msiba mazishi ijumaa hii nchini Denmrak

 Tanzia/ Funeral
Tunawatangazia wa Tanzania wote kutakuwa na maziko ya Mtanzania mwenzetu Bi Fawzia Diwani Mathiesen kilichotokea Kolding Sygehus Tareh 27/1/15
Baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Maziko yatafanyika Ijumaa Tarehe 30/1/15
Vejle Nordre kirkegård
Havelodden 4. Vejle.
Saa 4 Asubuhi.
Baada ya maziko kutakuwa na chakula na kuwapa mkono wa pole wafiliwa , katika anuan hii Olivenvej 65. 6000 Kolding . Ukiskia tangazo hili mjulishe mwenzio. Ahsanten sana.
Follow us on instagram swahili movies and Like our facebook pages Swahili movies.com and  for more updates about Swahili movies latest news, Scandal, Celebrities, features,european news, American,Australian ,Africa news, Music , news and more

CREDIT :   here

Tupe maoni yako hapo Chini..!!

 

 

MUME: ZARI HAWEZI KUZAA NA DIAMOND

Oohoo! Wakati staa mkubwa wa muziki wa Afro-Pop, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akichekelea kitendo cha mpenzi wake wa sasa, Zarinah Hassan ‘Zari’ au ‘The Boss Lady’ kunasa mimba yake, habari ya mjini huko Kampala, Uganda ni juu ya aliyekuwa mume wa mwanamama huyo, Ivan Ssemwanga kufunguka na kusema: “Naapa Zari hawezi kuzaa na Diamond.”
10903266_1517204571876514_1029472044_n
Staa mkubwa wa muziki wa Afro-Pop, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa na Zarinah Hassan,  ‘Zari’.
HABARI YA MJINI
Wikiendi iliyopita, vyombo vya habari na mitandao nchini Uganda ambako kuna makazi mengine ya Zari mbali na Afrika Kusini, kulipambwa na habari hizo baada ya mwanaume huyo aliyezaa na mwanamama huyo watoto watatu kuanika siri nzito juu ya ishu hiyo.
‘Ubuyu’ huo ulidadavua kwamba, kwanza jamaa huyo mwenye utajiri wa kutupwa alianza kwa kuelezea namna alivyoshtuka aliposikia Zari ni mjamzito.
ASHANGAA KUSIKIA ZARI MJAMZITO
Alisema kwamba alishangaa kusikia Zari ni mjamzito wakati ana umri wa karibia miaka 40 na watoto watatu ambao amekuwa akiwapuuza na kuendelea kuzurura na mpenzi wake mpya, Diamond sehemu mbalimbali ndani na nje ya Bara la Afrika.
mumewazari001
Ivan Ssemwanga akiwa na ‘Zari’
TATIZO UMRI?
Ilielezwa kwamba Ivan aliweka wazi kuwa amekuwa na hofu kwa kuwa Zari ni mwanamke ambaye umri umemtupa mkono hivyo anaweza akashindwa na ‘stresi’ za malezi ya mtoto mchanga.
Maoni ya Ivan ameyatoa baada ya Diamond kufichua kwamba Zari ni mjamzito huku akitupia vielelezo vya vipimo mitandaoni vikionesha kiumbe anayekua tumboni kwa mwanamke, jambo lililosababisha jamii kuamini kuwa ni Zari kwa kuwa wawili hao wamekuwa wakionekana kimahaba na kulala chumba kimoja kwenye hoteli mbalimbali.
Jamaa huyo alisema yeye ameshazaa na Zari watoto watatu na kwa pamoja walikubaliana kwamba Zari asilete kiumbe mwingine duniani.
NI AJABU?
Kwa mujibu wa Ivan, aligundua kwamba Zari hawezi kuwatunza vizuri watoto wake hivyo ni ajabu kuona anaongeza mwingine.
“Kwa ninavyomjua Zari, naapa hawezi kuzaa na Diamond,” alikaririwa jamaa huyo bila kufafanua kama mimba ambayo tayari Zari anayo itakwenda wapi.
oooi
Watoto wa Ivan Ssemwanga na ‘Zari’.
UMRI WA MWISHO KUZAA NI UPI?
Kutokana na maelezo ya Ivan, Ijumaa Wikienda liliingia mzigo kutaka kujua umri wa mwisho wa mwanamke kuzaa ni upi?
Kwa mujibu wa mtaalamu wetu, umri wa miaka 41 bado mwanamke ana uwezo wa kushika mimba kama hana matatizo yoyote ya kiafya ambayo yanaweza kuzuia kwa namna moja au nyingine asishike mimba.
Mara nyingi muda hasa wa mwisho kabisa ni umri wa miaka 45 endapo pia mwanamke anakuwa hana tatizo la kiafya.
Hata hivyo, umri mzuri wa mwisho wa kuzaa kwa mwanamke unaoshauriwa ni miaka 40 kwani nyonga zinakuwa zimeanza kuchoka hasa kama mama atakuwa amezaa kabla.
TURUDI KWA ZARI
Kwa maelezo ya mtaalam wetu, hata kama mwanamama huyo anakaribia umri wa miaka 40 si kigezo cha kushindwa kumzalia Diamond hivyo kinachohitajika ni uangalizi wa hali ya juu.

 

Follow us on instagram swahili movies and Like our facebook pages Swahili movies.com and  for more updates about Swahili movies latest news, Scandal, Celebrities, features,european news, American,Australian ,Africa news, Music , news and more

CREDIT :   Global .com

Tupe maoni yako hapo Chini..!!