Zimepita siku mbili sasa, baada ya msanii wa kundi la filamu NGG-Production nchini Holland Bethlehem Zelalem kwa jina maharufu Betty kusherekea sherehe ya kuzaliwa kwake. Msanii huyo ambaye mume wake ndiye rais wa kundi hilo, alipatwa na mshangao wa furaha baada ya baadhi ya wasanii wenzake kumletea keki na vinywaji nyumbani kwake na kusherekea naye kwa pamoja siku ya kuzaliwa kwake.
Timu ya Umoja Radio ilikutana na msanii huyo ana kwa ana ilikuhuliza namna alivyoandaa sherehe yake bila kujulisha watu wengine pamoja na Umoja Radio. Tulipo muhuliza alikuwa na haya machache ya kusema: ” Mimi mwenyewe sikutegemea sababu mpango wa kuhandaa sherehe sikukuwa nao labda watu wengine wanaweza kusema kwamba nimeandaa sherehe bila kuwahalika, hapana, hata mimi ilikuwa surprise kwangu kuona wanakundi wenzangu kuja nyumbani kwangu na kunifanyia kidogo waliyokuwa nayo kama ishara ya upendo. Nimewashukuru sana kwa kitendo walichokifanya sababu ni upendo uliyo mwingi kati yao kwangu na ndiyo maana wakahamua kunifanyia hivyo. Mungu awabariki”. Alisema Betty
Hapa chini mi baadhi ya picha za tukio
Follow us on instagram swahili movies and Like our facebook pages Swahili movies.com and for more updates about Swahili movies latest news, Scandal, Celebrities, features,european news, American,Australian ,Africa news, Music , news and more
CREDIT : Umoja radio
Tupe maoni yako hapo Chini..!!