DIAMOND AKANUSHA KUKATAA KUPOKEA MILIONI 500 ILI AMPIGIE KAMPENI LOWASA 2015

DAI
Meneja  wa msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Nasib Abdul ‘Diamond’, Babu Tale, amesema hawajawahi kupewa kiasi cha fedha Sh mil 500 na Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, ili wampigie kampeni za urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Akizungumza na Mpekuzi, Babu Tale alisema watakuwa wehu kukataa fedha nyingi kiasi hicho wakati wenyewe wanafanya muziki ili kupata fedha, lakini ukweli ni kwamba hawajapewa kitu chochote.
Alisema hata hivyo Diamond yupo tayari kumfanyia kampeni mgombea yeyote atakayetangazwa kuiwakilisha CCM.
“Kama kweli tungekataa fedha hizo hata Mwenyezi Mungu angetulaani, ila naamini taarifa hizo zitakuwa zinasambazwa na wapinzani wa kisiasa wa kiongozi huyo kwa  lengo la kumchafua, hajawahi kutupa ofa hiyo,”alisema Babu Tale.
Meneja huyo alitoa ufafanuzi huo baada ya hivi karibuni kuzagaa kwa taarifa ambazo si za kweli, kwamba walipokea kiasi hicho ili kumpigia kampeni Lowassa.
Follow us on instagram swahili movies and Like our facebook pages Swahili movies.com and  for more updates about Swahili movies latest news, Scandal, Celebrities, features,european news, American,Australian ,Africa news, Music , news and more

CREDIT :   Swahilione

Tupe maoni yako hapo Chini..!!