“Wote ni wajukuu zangu” – Mama Diamond baada ya Hamisa kujifungua mtoto

 

moja baada ya Mwanamitindo Hamisa Mobeto kujifungua mtoto wa kiume na story zikisambaa kuwa mtoto huyo ni mwimbaji staa wa Bongofleva Diamond Platnumz ingawa wenyewe wanazikanusha, sasa leo mama mzazi na dada wa Diamond wamefunguka.

Wakiongea kwenye na Soudy Brown kwenye U HEARD ya XXXL ya Clouds FM baada ya kuendelea kusambaa kwa taarifa hizo nao walifunguka.

>>>”Hamisa rafiki yangu siyo wifi yangu lazima niwe na furaha kwa sababu kajifungua salama. Wewe ulikuwa unataka nifanyeje? Hizo habari za Diamond mimi sizijui. Niulize mambo yangu. –  Esmaplatnumz

“Wewe unanitafuta nini Soudy? Naumwa kifua. Watoto wote ni wajukuu zangu hata wewe mtoto wako ukizaa mjukuu wangu. Wewe mwenyewe mwanangu, mtoto ukizaa mjukuu wangu. Wewe ni shushushu mbona hujafika Hospitali kumuona? Walioniona nimeenda Hospital waambie wakuhadithie vizuri. Mimi namuombea maisha mema alee mtoto wake vizuri kwa amani na furaha.” – Mama Diamond

Bonyeza Play hapa chini kusiliza FullStory.. USISAHAU KUSUBSCRIBE

https://www.youtube.com/watch?v=lK039oGTUpw&feature=youtu.be

 

 

Kesi ya Wema; Wakili Apinga Ushahidi wa Mkemia Mkuu

KESI inayomkabili staa wa Bongo Muvi, Wema Sepetu, imeahirishwa hadi Agosti 4 mwaka huu ambapo Hakimu Mkazi, Thomas Simba, atatoa ufafanuzi juu ya taarifa iliyosomwa na ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali.

 

Kesi hiyo imeahirishwa kutokana na wakili wa utetezi, Peter Kibatala, kusema ripoti hiyo ina mapungufu mengi ya kisheria na hivyo hakimu akawaomba mawakili pande zote mbili kuridhia apate muda wa kuipitia ili itakapoendelea aweze kuitolea ufafanuzi.

 

Awali, kesi hiyo iliahirishwa kusikilizwa kwa muda mahakamani hapo kutokana na wakili wa Wema kutokuwepo mahakamani hapo, ambapo imeanza kusikilizwa majira ya saa 6:30, leo mchana.

Wema na wenzake wanashtakiwa kwa kosa la kukutwa na kutumia bangi ambapo kesi hiyo itaendelea tena Agosti 4, 2017.

Na Denis Mtima/GPL

KUPATA HABARI NA MAISHA YA UGHAIBUNI BONYEZA HAPA CHINI ;KWENYE YOUTUBE CHANNEL YETU USISAHAU KUSUBSCRIBE