Mama yake Irene Uwoya amlilia Ndikumana

Mama mzazi wa msanii Irene Uwoya ambaye ni mkwe wa marehemu Hamad Ndikumana aliyefariki usiku wa jana kuamkia leo, ameshikwa na uchungu kwa kumwaga machozi mengi na kusema kabla marehemu hajafariki alikuwa anawasiliana naye na alimtaka kuwa na subira
Akiongea huku akilia kwa kwikwi na machozi yakimtoka, mama Uwoya amesema Ndikumana alikuwa ni zaidi ya mkwe kwake, na waliishi vizuri siku zote, na kumtia moyo kuwa atayavumilia yote ambayo alikuwa akiyapitia.

“Ndikumana mimi sijui nianzie wapi, alikuwa mkwe wangu kipenzi alikuwa kama rafiki, alivuka hata ukwe, Ndikumana wangu mkwe wangu siku zote tumeishi nae vizuri, siku zote tumekuwa tukiwasiliana mpaka mwishoni hapa nilikuwa natoka safari, ananiambia mama naomba tuwe na moyo wa subira, mimi nitavumilia yote ya dunia lakini mimi ni mwanao mpaka naingia kaburini, na kweli mpaka anaingia kaburini, mwanangu mimi nilikuwa nampenda”, alisikika mama yake Irene Uwoya ambaye alikuwa akilia kwa uchungu.

Ndikumana alikuwa mume wa ndoa wa msanii Irene Uwoya na baadaye walitengana, na kisha Irene Uwoya kuolewa na msanii wa bongo Fleva Dogo Janja.


Lulu Awaambia Ndugu Zake Wasikate Rufaa Kilichotokea ni Mipango ya Mungu

Imeelezwa kuwa baada ya msanii Elizabeth Michael kusomewa hukumu ya kifungo cha miaka miwili jela, aliwaambia ndugu zake wasikate rufaa kwa kuwa kilichotokea ni mipango ya Mungu na yupo tayari kukabiliana nayo.

Msanii wa wa Maigizo Elizabeth Michael akiwa ndani ya chumba cha mahakama kuu jijini Dar .Picha nyingine lulu akipandishwa katika gari ya polisi baada ya kuhukumiwa .Picha na Omary Fungo

Msanii , Muhsin Awadh maarufu Dk Cheni ambaye amekuwa karibu na mwigizaji huyo katika kipindi chote amesimulia hali ilivyokuwa muda mfupi baada ya jaji kutoa hukumu hiyo.

“Kusema ukweli Lulu alijua lolote linaweza kutokea ila la kufungwa ni kama hakulipa kipaumbele sana, jaji alipomaliza kusoma hukumu alishtuka kama sisi wengine wote lakini ajabu alikuwa wa kwanza kurudi katika hali ya kawaida na kutoa kauli za ujasiri,” anasimulia Dk Cheni

Lulu alisema: “Sipingani na maamuzi ya Mungu, haya ni maamuzi yake na nimekubaliana nayo. Ana makusudi yake kunipa hiki kilichotokea leo”.

Anasema kingine alichowaambia ni kuachana na masuala ya kukata rufaa kwa sababu bado hatakuwa huru: “Acheni miaka miwili siyo mingi, sitaki kupingana na mahakama , naheshimu maamuzi ya mahakama, acheni nitumikie kifungo changu. ”

Mapema wiki hii mwigizaji huyo alihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela baada ya kupatikana na hatia ya kumuua bila kukusudia mwigizaji mwenzake Steven Kanumba, Aprili 7,2012.

SWAHILIMOVIES INAMPA POLE SANA LULU