Mashabiki wamchana Alikiba na kumtaka asijihusishe na siasa la sivyo !

Mashabiki wamchana Alikiba na kumtaka asijihusishe na siasa la sivyo wataacha kusapoti kazi zake, ni baada ya kumpost Mkuu wa mkoa wa Arusha.
.
kupitia mitandao yake ya kijamii aliweka video ya Mrisho Gambo akisisitiza wananchi juu ya umuhimu wa kulipa kodi na kudai risiti pindi wanaponunua bidhaa mbalimbali ili kuiwezesha serikali kupata mapato.
.
Kitendo hicho alichofanya Alikiba kimewafanya fans wake wengi kutofurahishwa hivyo kumtolea uvivu huku wengine wakienda mbali zaidi na kumtaka msanii huyo asijihusishe kabisaa na masuala ya siasa la sivyo wataacha kuanza kusapoti kazi zake, japo wapo baadhi yao hawakuona tatizo msanii huyo kuweka video hiyo.

credit- trim saleem follow instagram swahili-world

xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx





Wolper achumbiwa ? Agawa madongo kwa Harmonize na Sarah

Wolper achumbiwa ? Agawa madongo kwa Harmonize na Sarah

.
“Nashukuru sana Mungu kwa kuniamini na kwa kuwa na mm na kuamua kutaka kubadilisha historia ya maisha yangu,ww ni mwanaume ambae umejitoa ili tu niwe wako,umetaka tufike mbali kwanza kabla ya mambo mengine (uwende kwa wazazi,(NDOA) pamoja na kwamba mahusiano yangu ya nyuma yalikuwa yana misuko suko mingi ila ww ni mwanaume ambae umemthamini

Jacq,Nilipotoka niliteswa sn na mapnz yaani Usaliti,Dharau,kukosa mapnz ya dhati etc Pamoja ya kuwa pia alishatokea mmakonde na kunipeleka mpk mtwara na matembele nikachuma na wanakijiji kunipokea na kupikia familia na kutambulishwa kwa wazazi lkn sikufanikiwa kufikia hatua hii ambayo ww umefika!Umenijali na umenisikiliza nilipokwambia sihitaji mtu

bali nahitaji future husband!Umekubali maamuzi yangu nilipokwambia km kweli unanipenda uende kwa wazazi nikijua ni mtego mkubwa nimekupa kumbe ww ndo kitu ulikua unakitaka kwangu?Nashukuru sn Mungu kwa kunifunza kunyamaza ktk haya mahusiano kati ya mm na ww,Can’t wait kesho moshi watakavyompokea mkwe wao kwa ajili ya mahari na kila kitu!(Ni mbege tu) Najiona mwenye bahati sn kumaliza mwaka kiaina hii na kuanza pia mwaka nikiwa na wewe…

.!Mungu akubariki kwa kuniamini na kuniona nitafaa nikiwa mkeo,Nyie dunia hii wakati wao waliniona sifai wakaenda kufata pesa,wanawake kuwatongoza na kuanza kunibadilikia lkn leo nimekupata ww ambae unaniuliza mbona walikuumiza sn na haukutakiwa kuumizwa,msemo wako mkubwa unaniambiaga nastahili kila kitu kizuri ktk hii dunia na sio maumivu…Nweiz staki kusema mengi lkn Namshukuru Mungu kwa kunipa wewe…!Sema wambea msijichoshe huyu sasa hayupo insta wala hajui haya mambo…!” Amesema Wolper

CREDIT: TRIM SALEEM INSTAGRAM FOLLOW INSTAGRAM SWAHILI-WORLD
XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX
KUFATILIA MAISHA YA UGHAIBUNI SUBSCRIBE CHANELI HAPA CHINI