Familia Yawakalisha Zari na Mobeto.

DAR ES SALAAM: Warembo waliokuwa kwenye vita ya maneno, Hamisa Mobeto na Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ wamedaiwa kuwekwa kitimoto ili waache kurushiana maneno kwenye mitandao ya kijamii.

Risasi Jumamosi limeelezwa kuwa, kwa nyakati tofauti wawili hao waliwekwa kitimoto na ndugu wa msanii wa Mzazi Mwenzao na kutakiwa waache malumbano hayo mitandaoni kwani hayaleti picha nzuri kwao na ukizingatia kosa limeshafanyika na msanii kukiri hadharani.

“Walichoelezwa tu ni kwamba, waache kutupiana vijembe mitandaoni maana wao sasa hata kama hawatakuwa wake wenza lakini tayari msanii ana damu yake kwa Mobeto. Amekiri kwamba aliteleza na kujikuta ameingia kwenye uhusiano naye hadi kufikia hatua ya kupata mtoto.