Aunt Ezekiel: Filamu hazilipi.Sapoti ya waume au wapenzi ndio inasaidia.

 

10501651_905523109462182_7997062673432426657_n

STAA wa filamu za Bongo, Aunt Ezekiel, amesema mafanikio ya wasanii wengi wa kike hayatokani na mauzo ya kazi hiyo bali sapoti ya waume au wapenzi wao kwa kuwa soko la filamu limeharibika.

“Filamu kwa Tanzania hakuna soko, walau wanaume, si wanawake, huwezi kunilinganisha mimi na Ray… Mimi kama si kuwa mwanamke, sidhani kama leo hii bado ningekuwepo katika filamu, kwa sababu kwa kiasi kikubwa nategemea sapoti ya wadau wangu, si mauzo ya filamu,” alisema.

Aunt alisema tatizo jingine katika soko la filamu nchini, ni wasanii kutopendana hali ambayo inashusha tasnia kila kukicha. Kwamba wangekuwa na mshikamano, wangeweza kufanya kitu cha kuwasaidia katika kuiboresha.

“Umoja ndiyo kila kitu hata kama tutakuwa hatuna hela, lakini tukikaa watu wengi kujadili kitu fulani, tutajua tufanye nini, hata kimawazo tu tutaendelea,” alisema

Follow us on instagram swahili movies and Like our facebook pages Swahili movies.com and  for more updates about Swahili movies latest news, Scandal, Celebrities, features,european news, American,Australian ,Africa news, Music , news and more

CREDIT :Bongo movies .com

Tupe maoni yako hapo Chini..!!