Category Archives: NEWS

BREAKING NEWS: BABU SEYA ACHIWA HURU NA RAIS MAGUFULI

Yametimia katika sherehe za Uhuru 2017. Katiba ya JMT Ibara ya 45 yatumika.
Karibuni kwa maoni

Rais John Magufuli akiwa kwenye kilele cha miaka 56 ya Uhuru amesemehe wafungwa 63 waliohukumiwa kwa vifungo mbalimbali na kunyongwa.

Miongoni mwa waliosamehewa ni wanamuziki Nguza Viking Alias maarufu Kama Babu Seya na Johnson Nguza(Papii Kocha) ambao walihukumiwa kifungo Cha maisha gerezeni kwa kosa la kubaka na kulawiti watoto 10 mwaka 2003 na kuhukumiwa Juni 25, 2004.

Pia Rais Magufuli amemsamehe mzee Matonya mwenye miaka 85 ambae alihukumiwa kunyongwa na ameshakaa miaka 37 baada ya hukumu na miaka Saba mahabusu.

XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX

Lulu Awaambia Ndugu Zake Wasikate Rufaa Kilichotokea ni Mipango ya Mungu

Imeelezwa kuwa baada ya msanii Elizabeth Michael kusomewa hukumu ya kifungo cha miaka miwili jela, aliwaambia ndugu zake wasikate rufaa kwa kuwa kilichotokea ni mipango ya Mungu na yupo tayari kukabiliana nayo.

Msanii wa wa Maigizo Elizabeth Michael akiwa ndani ya chumba cha mahakama kuu jijini Dar .Picha nyingine lulu akipandishwa katika gari ya polisi baada ya kuhukumiwa .Picha na Omary Fungo

Msanii , Muhsin Awadh maarufu Dk Cheni ambaye amekuwa karibu na mwigizaji huyo katika kipindi chote amesimulia hali ilivyokuwa muda mfupi baada ya jaji kutoa hukumu hiyo.

“Kusema ukweli Lulu alijua lolote linaweza kutokea ila la kufungwa ni kama hakulipa kipaumbele sana, jaji alipomaliza kusoma hukumu alishtuka kama sisi wengine wote lakini ajabu alikuwa wa kwanza kurudi katika hali ya kawaida na kutoa kauli za ujasiri,” anasimulia Dk Cheni

Lulu alisema: “Sipingani na maamuzi ya Mungu, haya ni maamuzi yake na nimekubaliana nayo. Ana makusudi yake kunipa hiki kilichotokea leo”.

Anasema kingine alichowaambia ni kuachana na masuala ya kukata rufaa kwa sababu bado hatakuwa huru: “Acheni miaka miwili siyo mingi, sitaki kupingana na mahakama , naheshimu maamuzi ya mahakama, acheni nitumikie kifungo changu. ”

Mapema wiki hii mwigizaji huyo alihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela baada ya kupatikana na hatia ya kumuua bila kukusudia mwigizaji mwenzake Steven Kanumba, Aprili 7,2012.

SWAHILIMOVIES INAMPA POLE SANA LULU