DK Cheni adai filamu yake ‘Nimekubali Kuolewa’ haichochei ushoga kama bodi ya filamu ilivyoichukulia na kuamua kuizuia

Uamuzi wa bodi ya Filamu Tanzania (TFB) kuizuia filamu ya muigizaji wa kiume na mkongwe, Dk Cheni ‘Nimekubali Kuolewa’, kwa madai ya kukiuka maadili na kuchochea tabia za ushoga, umepingwa na msanii huyo ambaye anaamini kabisa kuwa maudhui ya filamu hiyo yangeelisha jamii zaidi ya picha katika cover yake.

Dk Cheni ameiambia Global Publishers kuwa picha iliyoko kwenye bango la filamu hiyo inayomuonesha akiwa amevaa shera, ndiyo iliyotumiwa na TFB kama kigezo zaidi huku mahudhui yakiwekwa kando.

“Eti ushoga wangu uko kwenye kujiremba sana, wamenionea, lengo letu ni kukemea na kupinga vikali vitendo vya ushoga na ndoa za jinsia moja, huwezi kuelimisha bila kuonesha madhara yake kwa vitendo kama ilivyo kwenye filamu hiyo. Amesema Dk Cheni.

Msanii huyo alivitaja vipande ambavyo anaamini ilibidi vifikiriwe na TFB kufunika sababu zao zilizopelekea kuzuiwa kwa filamu hiyo.

duuu_fullDoctor Cheni na movie yake mpya

“Lakini ndani ya filamu hiyo, kuna kipande ambacho kinaonesha kiongozi wa serikali akikemea kitendo hicho, sasa hapo ushoga wangu uko wapi? Kuvaa shera kwenye cover? Alihoji Dr. Cheni na kusisitiza kuwa uamuzi huo haukuwa sahihi.

Mwaka jana Dr. Cheni aliiambia tovuti ya Times Fm kupitia kipengele cha Times Q & A ambapo alisema kuwa anatarajia kufanya filamu hiyo ambayo itakuwa ya tofauti ama ya pekee (unique) zaidi.

“Nahisi filamu inayokuja inaitwa ‘Nimekubali Kuolewa’, itakuwa ya kipekee sana, kwa sababu hata pale kwenye cover lake tu itakuwa ‘unique’ kwa sababu ntakuwa nimekaa nimevalishwa shela, kuonesha kwamba ni kweli nimekubali kuolewa, hii itakuwa tofauti na movie nyingi nilizowahi kucheza, itakuwa ‘Unique’.” Dk Cheni aliiambia tovuti ya Times Fm.

Usisahau kulike and share pia unatupata facebook .  swahili movies .com
pia follow us instagram  swahilimovies