KIMENUKA! Cloud Amfanyia Fitna Frank Mwikongi Deal La Kwenda Kufanya Filamu Uingereza, Ushahidi Wasambaa.

10710817_951617761519383_9079778302197319373_n

Mambo hadharani !…Haya ni mapya yameibuka leo bila chenga. muigizaji wa filamu nchini Issa Musa “Cloud 112” anadaiwa kumfanyia fitna na majungu star mwenzake wa filamu nchini Frank Mohamed Mwikongi katika deal la kucheza filamu lililotokea nchini Uingereza hivi karibuni.
Kwa ,mujibu wa Didas Fashions ambaye ndiye mtengenezaji wa filamu hiyo ya Mateso Yangu Ughaibuni chaguo la kwanza la filamu hiyo alikuwa ni Frank Mwikongi na walizungumza mwanzo na kuafikiana Frank alipwe mil.2 kama gharama za kucgheza movie hiyo pekee lakini baadaye Cloud akaingia kati na kutaka yeye hiyo nafasi huku akidaiwa kumwambia Didasfacions kuwa Frank hawezi kuigiza wala kuongoza filamu(Ukweli ni kuwa Frank ana kipaji kikubwa cha kuigiza pengine kumzidi Cloud)  kwa hiyo apewe yeye kazi ataifanya hata bure. Soma alichoandika Didas upate undani zaidi.

10649778_951618161519343_2518388080246736831_n

Jamani mnamuona huyu kaka hapa?(Frank )Huyu kaka anaitwa Frank kwa wale msiomjua. Huyu kaka ndio alikuwa aje UK kucheza movie ya MATESO YANGU UGHAIBUNI. Na tulisha kubaliana hadi bei maskini na kila kitu kilikuwa poa. Mara ghafla nikapokea simu ya kinafki, na wakati huo mie nilikuwa sijui lolote kuhusu bongo movie. Nikaambiwa huyu kaka ninae taka kumchukua hajui kucheza wala ku direct movie. Nika-pampiwa vibaya mnoo mpaka nikatia akili. Frank popote ulipo naomba unisamehe najua ulikuwa tayari umekuwa na tamaa ya safari ya kuja ulaya, ila waziba rizki wakafanya yao. Wacha naishi hapo. Hii ni intro tu. Hadithi kamili inakuja. Kaeni na ndimu zenu”

Baada ya muda kidogo tena Didasfacions akafunguka tena Instagram kwa kuandika.

“Haya uliniita mimi tapeli tena mdhulumati, nimekudhulumu million 8 za kuja kucheza movie, ukaenda mpaka kwenye magazeti kusema, nikapigiwa na wenye magazeti, nikawapa ukweli na ushahidi. Tena huu ni mfano tu, ninazo nyingi na za aibu, na bado naendelea. Frank aliniomba nimlipe Tsh 2 million kucheza hiyo movie, nikakubali, wewe ukasema kila kitu utafanya bure ila nikisha uza movie nikufikirie, sasa leo umemfanya Steve Nyerere kajiuzulu eti kisa kanisaidia uzinduzi, na hela ya PSPF tumekula, huu ni mfano nakuja kumwaga mengi. Ulijitolea kila kitu bure uje ulaya, leo umenipaka mavi dunia nzima mimi tapeli, unawafanyia fitna watu wote wanao kaa karibu na mimi. Hii ni haki? Sawa mimi tapeli dhulumati, zote ni njia za kutafuta riziki. Tutafika hata mahakamani. Bado na rudi na mazito zaidi. Ongezeni ndimu”

Itaendelea kadri Didasfacions atakavyofunguka………… but moja ya mawasiliano ya Didasfacion na Cloud hayo hapo juu.
Filamu ya Mateso Yangu Ughaibuni ilichezwa na Cloud, Monalisa, Riyama Ally na Wastara na ilizinduliwa hivi karibuni viwanja vya Leaders, Dar es salaam.

Follow us on instagram swahili movies and Like our facebook pages Swahili movies.com and  for more updates about Swahili movies latest news, Scandal, Celebrities, features,european news, American,Australian ,Africa news, Music , news and more

CREDIT : http://www.bongomovies.com

Tupe maoni yako hapo Chini..!!