Mashabiki wamchana Alikiba na kumtaka asijihusishe na siasa la sivyo !

Mashabiki wamchana Alikiba na kumtaka asijihusishe na siasa la sivyo wataacha kusapoti kazi zake, ni baada ya kumpost Mkuu wa mkoa wa Arusha.
.
kupitia mitandao yake ya kijamii aliweka video ya Mrisho Gambo akisisitiza wananchi juu ya umuhimu wa kulipa kodi na kudai risiti pindi wanaponunua bidhaa mbalimbali ili kuiwezesha serikali kupata mapato.
.
Kitendo hicho alichofanya Alikiba kimewafanya fans wake wengi kutofurahishwa hivyo kumtolea uvivu huku wengine wakienda mbali zaidi na kumtaka msanii huyo asijihusishe kabisaa na masuala ya siasa la sivyo wataacha kuanza kusapoti kazi zake, japo wapo baadhi yao hawakuona tatizo msanii huyo kuweka video hiyo.

credit- trim saleem follow instagram swahili-world

xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx