Kutana na Songa Media Group , ni kikundi cha sanaa ambacho kinafanya shughuli za film za kiswahili na kiingereza huko Noxville Tennesee Marekani , ni kikundi kinachokuja kasi nchini marekani na mpaka asasa kimeshafanya film zaidi ya kumi kama , “No way out, Death by love, 30 minute to live . Siri ya mafanikio , Turn up, Salome, na nyingine nyingi nilipata bahati ya kuongea na Director wa kundi hilo Remi J Machali na alikuwa na haya ya kusema
Remi J Machali Director of Songa Media , Pajero J Machali
Mimi ndie Director wa kundi hili Pia tuna Pajero J machali ni Manager na Sheba J Machali ndio President wa kundi hili la Songa Media lenye wasanii wa kike 20 na wakiume 30 nashukuru Mungu kwa kulifikisha hapa hili kundi ambalo lilianza mwaka 2012, lakini nashukuru kwa washabiki wetu wametupokea vizuri filamu zetu za kiswahili na kiingereza marekani na duniani kote na tunawaahidi mashabiki tutafika holywood
MATATIZO GANI YANAYOWAKABILI
Matatizo ni mengi , kwa kweli kuanzia casting, location, location managing, Writing can be little difficult plus working with people with nasty personalities. but i’m always finish my work
MNA WASANII WAKIKE ZAIDI YA 20 MBONA MNAWATUMIA SANA 2 AU 3
Hatuwezi chukua au kumtumia kila msanii kwenye movie sababu tu ni mrembo au yuko kwenye kundi ,bali tunaangalia nani aliye bora kiwango cha uchezaji , anayemudu kucheza vizuri , sababu mwisho wa siku hii ni kazi na inatakiwa iuzwe . ndio maana unakuta msanii mmoja au wawili wanacheza kila movie
NYINYI MNA MPANGO WA KUFANYA KAZI NA HOLYWOOD NA WATU 13 KATI YA 50 MMESOMA FILM SCHOOL TENA MNAISHI MAREKANI , KITU GANI KINAWAZUIA MSIENDE SASA HOLYWOOD
Ni elimu , ili tuweze kufanya kazi holywood tunaitaji elimu ya kutosha kwani kipaji peke yake hakitoshi , na watu hao 13 wanaosoma film school hawajamaliza hivyo tukienda hatutafanya movie nyingi wala kupata pesa nzuri.
ASANTE SANA MNA LOLOTE LA KUAMBIA MASHABIKI WENU
Tunawapenda sana mashabiki wetu tunawatakia heri ya mwaka mpya na wajiandae mwaka mpya umeanza na mambo mapya , wakae mkao wa kula film yetu inakuja soon.
Siam J. Manuels , Pajero J Machali and Conley Bunch
Usisahau kulike and share pia unatupata facebook swahili movies .com
pia unaweza follow us on instagram. swahilimovies