Wema Sepetu Aanawashangaa wanaomponda Jokate

Wema

Wema Sepetu, amewashangaa wanaomponda Jokate Mwegelo baada ya kumaliza tofauti zao, asema wanaingilia uhuru wa wasanii hao.

1656009_800091570005337_1230942157_n

WEMA SEPETU  NA JOKATE MWEGELO

Mwigizaji Wema Sepetu, amewashangaa wanaomponda Jokate Mwegelo kwa kumaliza tofauti baina yao akisema kuwa hawatendi haki na wanaingilia uhuru wa wasanii hao.

Kauli ya Wema imekuja siku chache baada ya Jokate kufika kwa kushtukiza katika onyesho lililofanywa na Wema mkoani Arusha hivi karibuni na kumaliza tofauti zao.

Wawili hao wanadaiwa walikuwa wakimgombea mwanamuziki nyota na tajiri, Diamond Platinum.

“Sikuona kioja wala ajabu, kwa kuwa tulikuwa marafiki na kilichotokea ni ujana. Kila mmoja amekaa na kuona hakuna haja ya kuwa na bifu zisizokuwa na faida. Nimemuunga mkono Jokate kwa kuwa ameonyesha kukua na kukomaa kiuamuzi, hakuna haja ya kumbeza kwa maneno ya kijinga,”alisema Wema.

Follow us on instagram swahili movies and Like our facebook pages Swahili movies.com and  for more updates about Swahili movies latest news, Scandal, Celebrities, features,european news, American,Australian ,Africa news, Music , news and more