JINA KAMILI UNAITWA NANI
Naitwa Rehema Amiry Nkalami natokea Tanga Tanzania .Ila naishi silkeborg Denmark ni mtangazaji wa swahili talk radio.
http://www.shoutcast.com/Internet-Radio/swahili%20talk%20radio
Hongera sana kwa kazi yako nzuri ya utangazaji, sasa ningependa kufahamu hii kazi ulianza lini
Asante sana , hii kazi ya utangazaji niliianza mwaka 2012 . sifanyi hii kazi sababu napenda utangazaji tu ,hapana bali napenda kuutangaza Uafrika pamoja na lengo la kukuza lugha za kiswahili na utamaduni wa mwafrika ulaya na nchi zote ulimwenguni.
Rehema akiwa na kikundi cha African Umoja Denmark kwenye sherehe ya utamaduni
Rehema akitangaza mavazi ya kiafrica kwenye Swahili talk radio
Unaweza vipi kufanya hii kazi ukizingatia wewe upo ugenini
Siku zote mtu anayenitia nguvu ni mme wangu mpendwa Søren . Yeye ni muandishi wa habari pia ni mtangazaji wa denish radio station,
lakini pia mimi nina studio yangu hapa silkeborg na zaidi nafanya kazi na jamii ya waafrica, pia watu wote ambao wanapenda kuongelea mambo yanayohusu Africa wanakaribishwa studio.
Rehema akiwa studio na Leonidas kwenye kipindi cha biblia
Rehema akimuhoji Mr Nice mwanamziki kutoka Tanzania
Hongera sana kwa kazi zako nzuri, sasa ningependa kujua mipango yako ya baadae.
Mipango yangu ni kuanzisha Tv talk show ambayo itaitwa REHEMA SHOW na kwa sasa maandalizi yote yameshakamilika ,niko kwenye hatua za mwisho ili kuanza kazi hiyo, na sababu mimi nitakuwa busy na talk show hivyo natafuta msaidizi kwenye radio mwezi wa pili ,mtu mwenye kipaji cha kuongea hasa kipindi cha kuchekesha
Rehema akiwa na Lucy Komba muigizaji toka Tanzania
Rehema akimuoji Raisi wa v.a.d film production Mr Safari Lukeka
Hongera sana dada Rehema kwa kazi nzuri unazozifanya ikiwa si tu kwa utangazaji bali hata kuutangaza uafrika pia kushughulika na mambo yanayousu jamii ya waafrica , Swahili movies inakupongeza na kushukuru kwa ushirikiano wako .
Usisahau kulike and share faceboook page yetu swahili movies .com