Big jj awataka wasanii waache roho ya wivu

Big JJ Muigizaji na mmiliki wa kampuni ya  Big JJ FILM PRO anayefanya vizuri scandinavia na Ulaya kwa ujumla kwa kazi zake nzuri za film  , amefikia hatua ya kuwataka wasanii wenzake kuacha wivu baada ya tatizo kubwa kutokea,    Big Jj alisema kuwa yeye anaweka Video kwenye youtube kusudi mashabiki wake waelimike na kuburudika bure kabisa ,

324691_250272421688331_819963892_o

lakini anasema waigizaji hawapendani baada ya kupata ujumbe kutoka kwa kampuni ya youtube  kuwa kuna watu wamelipoti kuwa video yake ni spam na kupelekea filamu hiyo kufungiwa ikiwa tayari mamilioni ya watu wameangalia, kikendo hiki hakikufurahishwa hata kidogo na Msanii huyu BiG JJ na ndipo alipoamua kutengeneza video ili kutoa ujumbe kwa wasanii wote kwa lengo la kuonyesha kuwa alichofanyiwa si sahhihi bonyeza hapa kuangalia hiyo video

https://www.youtube.com/watch?v=Fh_cLKNDa3c

 USHAURI KUTOKA SWAHILI MOVIES KWA WASANII  TUJIKUMBUSHE

Tukio hili sio mara ya kwanza kutokea huku ulaya kwani kutokana na makundi kuongezeka na kuwa na ushindani wa kikazi mkubwa unaoendelea kwa sasa kitendo cha kufungiana filamu youtube au trailer kimekua kikubwa sana na hata siku za nyuma kampuni ya VAD Ilishalalamika kufanyiwa kitendo kama hiki,

USHAURI

kufungiana Video sio solution ya kumshusha mtu au mtengenezaji FILM  kwani baada ya muda ataiweka na mashabiki wake watarudi palepale ila si jambo la kiungwana kwa nyinyi mnaofanya vitendo hivyo muwe ni wasanii au watengenezaji filamu au tu watu binafsi kitendo hiki sio kizuri kwani malipo ni hapa hapa duniani unapomsumbua mtu anayepoteza muda wake Mungu hakika atakulipa , bali kama wewe kundi lako au kazi zako unataka zipande kwa nini usifanye kazi bora na nzuri , au kuomba msaada kwa Big jj au makundi mengine usaidiwe .

885869_478841275498110_2004588571_oBig JJ on action

Follow us on instagram swahili movies and Like our facebook pages Swahili movies.com and  for more updates about Swahili movies latest news, Scandal, Celebrities, features,european news, American,Australian ,Africa news, Music , news and more

Hatimaye Ashley Toto amjibu Lucy Komba usiende ugenini ukajifanya wewe ndio mwenyeji

LUCYF.K.PIC071lucy komba

TUJIKUMBUSHE KWA KIFUPI

Hivi karibuni Star mkubwa wa filamu za Swahiliwood Lucy Komba alidaiwa kumnanga muigizaji chipukizi toka Kenya anayeishi Ujerumani Ashley Toto muigizaji wa VAD wakati akifanyiwa interview na Swahili talk radio ya nchini Denmark. Chanzo kimoja kikizungumza na Swahiliworldplanet “Lucy kafanya Interview na radio moja hapa Europe… So kaongea kama vile anamchukia au ana beef flani hivi na Ashley Toto, kasema eti amekuja Europe na akaambiwa kuna mastaa now hapa Europe na wana majina makubwa…akataka kuona hiyo movie aloigiza Ashley, alipoona akasema hakuna kazi yoyote hapa ni kelele tu kapiga na scandals nyingi wala hana lolote…. So watu wengi wameanza kumuuliza Ashley kama ana beef na Lucy ila hajaongea kitu”


Baada ya kuzipata habari hizo ilibidi kumsaka lucy lakini hakuwa hewani kwa muda huo kwa hiyo ilibidi kumsaka msanii mwingine ambaye alihusika pia katika interview hiyo na kuulizwa kama Lucy alimtemea nyongo Ashley au lah jibu lake lilikuwa “Sio kweli kabisa Lucy hajamponda Ashley Toto wala hata kumtaja kwa jina au kwa namna yoyote ile….sio kweli kabisa” alisisitiza msanii huyo

Hata hivyo baadaye Lucy akawa hewani na alipoelezwa kuhusu kumchana radioni Ashley Toto star huyo wa muda mrefu na mwenye uwezo wa kuuva uhusika katika filamu alisema”ha ha ha sijamponda nani kakwambia yeye mwenyewe? sijampoda ila aliniuliza niwashauri nini wasanii wa huku nikamwambia wafanye kazi siyo mtu anacheza scene moja anaanza kujitangazia ustar watu wanatakiwa waone nini msanii kafanya ndiyo wampe sifa hiyo ndo kazi ya sanaa lakini sijaponda yeyote wala sijataja jina la yeyote mbona wasanii wa hivyo wako wengi lakini nashangaa watu wanapenda umaarufu au wanapenda ugombana au kujibizana na mastar ili wawe mastar kupitia sisi kuna mwingine nae analalamika eti mimi nimemponda siyo huyo tu wanajoshtukia na kama wanahizo tabia kweli waache”

Lucy ambaye anasifika nchini Tanzania kwa kujipatia umaarufu kutokana na filamu zake na sio skendo kama baadhi ya mastaa wenzake walivyo alisema kuwa hata hamjui huyo Ashley “Ila huyo msanii mimi simjui wala sijawahi kuona kazi alizocheza na pia waache kujitangazia u-star.  U-star unakuja wenyewe taratibu siyo wa kujilazimisha aache kelele afanye kazi watu waone, mastar wenyewe wamekaa kimya”

Star huyo wa filamu za Yolanda na Pretty Teacher alimalizia kwa kusema ” halafu kawaida yangu huwa sipendi mabifu na watu ndo maana huwa nakaa kimya ila wakinichokoza nitaongea, ila watu wanataka nicharuke maana kila ninachofanya wanaanza maneno nikicharuka hawatanishika waambie. huwa sipendi upumbavu…..waandikie ninachoongea. nimefunga mdomo.kwa muda mrefu ila mbwa ukimzoea anakufuata mpaka msikitini sasa sitaki mazoea na mbwa”

1452566_10202286076580892_1031232508_nAshley Toto

Baada ya kuona interview hiyo ndipo swahili movies ilipomfata Ashley Toto ambaye kwa muda wote alikuwa kimya na kutaka kujua hasa kuna nini kati yake na Lucy Komba kama mashabiki wengi wanavyotaka kujua .

 SM–   Mambp vp Toto

TOTO  -safi sijui nyie

SM  – niambie kuna kitu gani wewe na lucy komba

TOTO– Hahahahaha Eti Mimi na Lucy?  Sina hio time ya Kumfwatilia, Kile alichoongea anakijua yeye Sababu sisi hatujuani wala hatufwatani, Huyo MBWA aliemtaja anamjua yeye coz hakuna Mbwa atakae Kufwata kama Hakujui Lazima awe yuakujua ndio akufwate ….

SM–  wewe na lucy mmeshawai kuonana

 TOTO – Hehehehehe Wacha Kuonana hata Perfume yangu Haijui

SM – sasa haya mambo yote yameanzia wapi Ashley au wewe uliwai kumchukulia bwana wake embu funguka maana inaonekana kama kuna kitu kimejificha kati yenu eeeh embu tuambie ukweli tafadhali mashabiki wako wanataka kujua ukweli

TOTO– Ataa Sijavaa Kiatu Chake na Wala Njia aloipita yeye Haramu mimi Kupita

SM –  wewe kwa nini unafikiri lucy anakuongelea wewe

 TOTO -Siwezi Kusema Kaniongea Mimi ila ningependa kumwambia Usiende Ugenini Ukajifanya wewe Ndio Mwenyeji. ..  Sometimes  vizuri kuchunga Kauli.Ningepeda kumuuliza Kwanini aite Watu MBWA? Ama au  PAKA? Au Majina ya wanyama  gani? Kwanini atafute Biff? Alimuingilia Kaona hamuwezi sasa kanivamia Mimi, Nia yake nini? Anachotaka Haswa ni nini?Asikae Na Wivu wakati Watu katukuta….Ustar bongo Na kina Rihanna wajiite Kina Nani? Mbona hawaiti Watu MBWA? Asitafute BIFF Na Mimi Kashindwa Na Irene Uwoya Na Monalisa sasa anivamia Mimi? Hata asijaribu coz Nitamuosha Na Tabia zake alizokuja Kuzifanya Huku Europe,Nani Hazijui… “Usiungie katika Mji wa Watu Ukajifanya wewe Mwenyeji” She Have to Finnish Kesi zake Na Uwoya and Monalisa First Ndio Aanza Na Mimi… Na kwataarifa Yake Asizoe Kutukana Watu Asio Wajua

 

10150438_10202956119971558_1090765896_oAshley Toto

1947659_10202710494511075_1059320109_nAshley Toto

Follow us on instagram swahili movies and Like our facebook pages Swahili movies.com and  for more updates about Swahili movies latest news, Scandal, Celebrities, features,european news, American,Australian ,Africa news, Music , news and more