Muigizaji Abou Hermis Twaleeb amekava katika gazeti jipya la Movie Star ambalo litakuwa linakujia kila wiki na kitendo hiki kimekuja baada ya mashindano yaliyokuwa yanafanyika katika kinyanganyilo cha kumtafuta mkali wa kuigiza kati ya Abou Hermis Twaleeb na Muigizaji mwenzake Bjohn Mausa lakini kula za mashabiki zikampendekeza Abou Hermis Twaleeb ….. na kwa siku za baadae kava hili lina mpango wa kuanza kuchapishwa na kusambazwa hivyo wapenzi wa habari za swahili movies Diaspora mkae mkao wa kula
kushoto Abou Hermis Twaleeb kulia ni BJohn Mausa
Hii ndio kazi ya B JOHN MAUSA RIZIKI YA MNYONGE
Hii ndio kazi ya Abou Twaleeb AFRICAN BOY
HUU NDIO USHAURI ALIOTOWA KWA WAIGIZAJI WENZAKE BNAADA YA KUSHINDA ABOU
HERMIS TWALEEB
Ushauri wangu mkubwa kwa wasanii chipukizi (kama mimi) ni kuwa seriously na kazi zao pale wanapopata nafasi za kufanya hivyo, wasifanye kazi kwa ajili tu ya kujulikana na kupata majina makubwa…wafanye kazi nzuri,kwa bidii na kwa kujituma sana ili waendelee zaidi kiusanii.
PILI: ni UMOJA…wawe na ushirikiane na wasanii wenzao bila kujali NANI ZAIDI. Umoja ni silaha kubwa ya kujifunza mengi kwa kuwa kila binaadamu anacho ana mtazamo wake, mawazo yetu yako tofauti sana, na kama vile ambavyo mkubwa anaweza kumuongoza mdogo..basi mdogo nae aamini kuwa anao uwezo wa kumuongoza mkubwa ikiwa tu Umoja, Upendo, Busara na Heshima vitatawala kati yao na hapo MAENDELEO YATAPATIKANA….
La mwisho ningependa kuwashauri wasanii wote chipukizi WASIKATISHWE TAMAA kwa namna yeyote ile. Safari ya kuwa msanii ni ngumu sana na ina mitihani mingi sana ambayo inakutegemea wewe mwenyewe utapambana nayo vipi. Unaweza kufuatwa-fuatwa, kutukanwa, kudharauliwa, kusingiziwa mabaya, kuonekana haujuwi chochote, na hata wakati mwingine ukatamani ujitoe na kufuta ndoto zako kiusanii…Hakuna kilicho rahisi katika FANI yoyote na wengi wanakata tamaa kwa kufuata nani anasema nini na nami anataka nifanye nini..wewe jiamini na upiganie kile unachotaka wewe na siyo wanachotaka wengine kwa kuwa UKIFANIKIWA ni faida yako mwenyewe na wengine..hivyo wasanii chipukizi MSITATE TAMAA DAIMA….MUNGU ATAWAONGOZA..
Mwisho alimalizia kwa kuwashukuru mashabiki wake wote waliompigia kura na kusema kwa kufanya hivyo wameonyesha upendo na ushirikiano .
Follow us on instagram swahili movies and Like our facebook pages Swahili movies.com and for more updates about Swahili movies latest news, Scandal, Celebrities, features,european news, American,Australian ,Africa news, Music , news and more