Asante Sana kwa wanaonikubali,na wasiyo nikubali wasubiri, nitawaleteya mazuri adi watanikubali. Katika kipindi cha hivi karibuni Muigizaji Claurice safi ni mmoja kati ya waigizaji wakuu wa Tamthilia ya Mawenge ameonekana akiafanya vizuri na akiwa amebeba nafasi kubwa katika tamthilia hiyo , licha ya kuwa alishacheza filamu mbalimbali katika kundi hilo la VAD lakiniwengi walikuwa hawamfahamu mpaka katika tamthilia hii ya mawenge ambayo amecheza muuhusika mkuu ,
Mbali na uwezo wake mkubwa wa kuigiza katika tamthilia hiyo ambayo anaigiza kama mwanamke kipofu anaenyanyaswa na mme wake , mashabiki wengi wangependa kumjua kiundani kuhusu muigizaji huyu ndipo swahili movies tulipoamua kumtafuta na kufanya nae mahojiano fatilia hapo chini uweze kujua mengi kuhusu Muigizaji huyu matata kutoka kampuni yako kongwe V.A.D Film Production ya Denmark.
Mashabiki wanaona kazi zako nzuri na uwezo wako mkubwa katika uigizaji lakini hawajui jina lako halisi ni na umeanza lini shughuli hizi za uigizaji ?
Mimi majina yangu, yakuzaliwa ni safi Clarice Bernard. kazi yangu ya uigizaji nilianza toka mwaka2007 kwenye kikundi kimoja kilikuwa kinaitwa one love Kilichokuwa kusini mwa kongo UVIRA .
Kitu gani kimekuvutia kuingia katika Uigizaji ?
mimi kitu ambacho kilinivutiyaga zaidi kwenye uhigizaji ni nafsi yangu yenyewe kwanza, sababu kipindi nilikuwa mtoto nilianza kuigiza kanisani, piya na shuleni.nakipindi tamthilia zilianza kuchezwa,tanzania ndipo nilivutiwaga Sana nikasema lazima na mimi siku moja nije kuwa muigizaji, kipindi icho KIDEDEA, na MAMMBO HAYO walikuwa wamepamba moto.
Umeshafanya filamu au kazi ngapi Mpaka sasa waweza zitaja?
Nimesha fanya filamu zaidi ya saba nimefanya filamu nne Congo,1 one buy one ,Tueshimu wazazi, love, mapenzi ayachagui.kwa apa Denamrk nimecheza filamu, 3 sorry my wife, maisha ya ndotoni, na nimwamini nani?. Ila bado zipo zinafanyiwa editing, zipo njiani zinakuja.
Wewe na mme wako wote ni waigizaji katika kampuni moja je kuna matatizo yoyote mnayokumbana nayo mkiwa wote ni familia moja yanayotokana na sanaa ? pia siku chache zilizopita ilijifungua mtoto na kuna matatizo au changamoto zozote unazopata ukiwa shooting kama msanii na una mtoto mdogo labda kulia ?
Matatizo hayawezi yakakosa tukiwa tupo kazini. Ila siyo mara kwa Mara.Namshukuru mungu sababu mwanangu siyo mlizi Sana, uwa hasumbui kipindi cha shooting, ilo nasema Asante kwa mungu.
Nini mipango yako ya badae katika sanaaa na Kwa africa ni msanii gani mkubwa unaependa siku moja uje uigize nae ?
Namuomba mungu asaidie kikundi chetu cha V.A.D kiendelee zaidi na zaidi. Kingine napenda niwe muigizaji zaidi ya hapa nilipo.
Wasanii hote ambaho wanakipaji Chao, mimi siku moja natamani kuigiza nao.Kama nilivyo igiza na Lucy komba nimefurahi Sana nimejifunza mengi kutoka kwake.
Unaushauri gani kwa wasanii wenzako na kwa mashabiki wako ?
Wasanii Tuwe tu na upendo wa kweli, usiyo na chuki kwa ndani, na tuwe tunaungana mkono .wale ambao wametowa kazi,tuwe tunawasapoti, asante sana kwa mashabiki wangu wale wanaonikubali,na wasiyo nikubali wasubiri, nitawaleteya mazuri adi watanikubali.
MUIGIZAJI SAFI AKIWA KWENYE PICHA ZA POZI MBALIMBALI
Hizi ni baadhi ya picha za behind the scene za tamthilia ya Mawenge
Selembe Toko akiwa on set na muigizaji claurice
https://www.youtube.com/watch?v=kyCnCAU2nJE&feature=youtu.be
Follow us on instagram swahili movies and Like our facebook pages Swahili movies.com and for more updates about Swahili movies latest news, Scandal, Celebrities, features,european news, American,Australian ,Africa news, Music , news and more
CREDIT : Here
Tupe maoni yako hapo Chini..!!