All posts by swahili movies.com

kukariri script tatizo kubwa by frank salum

 Kutana na msanii Frank Salumu , muigizaji huyu ametokea congo ila anaishi denmark ni msanii ambaye nyota yake imengarakuanzia mwaka 2011 mpaka sasa bado ameweza kukaa juu kwenye kazi zake za film na kumfanya akubalike nchini denmark na nchi mbalimbali za ulaya  na hizi ni baadhi ya movies zilizomtambulisha msanii huyu    Dont look down to the poor, if i knew. Pasport Love.  Ahadi ,Moyo Wangu  na nyingine nyingi … pata mawili matatu kutoka kwake.

1010662_4606236888805_1854495159_nFrank Salum

HABARI YAKO

salama kabisa , nashukuru

HONGERA SANA KWA KUWEZA KUKAKA JUU TOKA 2011 MPAKA SASA,TUPE SIRI YA  MAFANIKIO

asante sana , siri ni kujituma , kufanya kazi kwa malengo na siku zote Mungu anakubaliki tu.

183647_4426367272177_1519825473_nFrank Salum na Ashley toto wakishuti Moyo Wangu Film

CHANGAMOTO GANI UNAPITIAKWENYE KAZI YAKO

Mimi siku zote ni mtu wa kazi , ila kukariri script ndio changamoto yangu kubwa ,   hahahahahah lakini siku zinavyozidi kwenda navyofanya kazi zaidi , nazidi kuwa mwepesi  na nawaahidi mashabiki wakae mkao wa kula , frank atakuja na mambo mapya, mwaka mpya mambo mapya wajiandae .

 

1527831_10200662380036776_2086888029_nFrank Salum

 

1521343_10200667178556736_254673398_nFrank Salum

1504015_10200671038573234_630830040_nFrank Salum akiwa location akifanya mambo yake

NINI MIPANGO YAKO YA BAADAE

Mipango yangu ni kuendelea kufanya kazi nzuri daima zitakazofundisha , kuelimisha na kuburudisha , kusonga mbele  zaidi  na kundi langu.

Swahili movies  inashukuru sana Frank sakum kwa ushirikiano wako.. tunakutakia kazi njema

Usisahau kulike and share pia unatupata facebook .  swahili movies .com
pia follow us instagram  swahilimovies

 

 

 

 

 

 

DIAMOND NOMA! KUMBE ALIMPITIA LULU!

Stori: Mayasa Mariwata STAA kiwango katika tasnia ya filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amekanusha uvumi uliozagaa mitaani kuhusu kutoka kimapenzi na mbabe wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’.

164292_147538705429101_598532288_nlulu

Imekuwepo minong’ono ya muda mrefu kitaani kuwa, Diamond analilia penzi la Lulu lakini Diamond au Sukari ya Warembo alipoulizwa kuhusu hilo, alisema siyo kwamba analilia tu bali waliwahi kutoka (haijulikani kwenda wapi) naye, madai yaliyotupiliwa mbali na Lulu.
MADAI YA AWALI
Habari zilizotua katika meza ya Risasi Mchanganyiko zinasema kwamba, wawili hao wanafanya kazi za kisanii pamoja (haikuwekwa wazi ni kazi gani kati ya filamu au muziki) lakini tatizo lililopo kati yao ni Diamond kumtaka Lulu.
Chanzo kilichoomba hifadhi ya jina lake, kilifunguka: “Diamond anashindwa kuelewa, tatizo yeye kila mwanamke anataka kutoka naye. Mwenzake anajua yupo kazini, yeye anataka penzi, ndiyo mzozo uliopo kati yao.”
diamond                                                                              Diamond

 

KAZI KWA DIAMOND
Paparazi wetu alimvutia waya Diamond ili kutaka kupata ufafanuzi kwa upande wake, ambapo aliposomewa maelezo yote alicheka sana kisha akasema: “Nililie penzi la Lulu? Acheni hizo… ngoja nikuambie kitu, siyo kulilia, mimi nimeshawahi kutoka naye. Nilitembea naye kishkaji tu kisha kila mmoja akaendelea na yake.
“Hayo mambo yalishapita na sikutaka kuyaongelea lakini kwa sababu naona kama yanakuzwa, ndiyo maana nimeamua kuweka wazi. Kwa sasa tunaheshimiana kama kaka na dada. Kuna ugumu gani mimi kuwa naye wakati nimeshampitia?”
Risasi: Unasema kweli Diamond?
Diamond: Wa asilimia mia moja.

 

LULURisasi: Una ushahidi gani?

Diamond: Watu wanaojua hii ishu ni wawili tu; Wema (Sepetu) na Penny (Penniel Mungilwa). Niliwaeleza kwa uwazi kabisa hawa ili tusielewane vibaya. Kama huamini waulize. Hawa ndiyo niliowapa siri hii.
Paparazi wetu alijaribu kuwatafuta Penny na Wema kupitia simu zao za mkononi lakini hawakupokea.
TURUDI KWA LULU SASA
Akizungumza kwa sauti ya kujiamini, Lulu alimshangaa Diamond na kusema kwamba, si kutoka naye tu bali hana hata kazi anayofanya naye pamoja.
“Nawashangaa sana eti mimi nifanye kazi na Diamond, kazi gani sasa wakati mimi na yeye tupo kwenye fani tofauti? Muziki na filamu wapi na wapi? Kifupi hayo madai hayana ukweli wowote na kila mtu yupo na yake,” alisema Lulu na kuongeza:
“Kwanza mimi siwezi kutoka na Diamond… levo zetu ni tofauti kabisa, wala hazilingani. Mimi nilianza kutoka kabla yake, nimeanza kujulikana toka kitambo hicho nina miaka mitano sijui hata kujifuta kamasi vizuri…. hakuna ukweli wowote.”
wema2                                                                     Wema sepetu
TUJIKUMBUSHE
Diamond amekuwa akihusishwa kutoka kimapenzi na mastaa mbalimbali, huku madai hayo yeye mwenyewe akiyakubali, jambo lililosababisha aitwe Sukari ya Warembo.
Penny                                                                                Penny
Mbali na orodha ndefu aliyotoka nayo Diamond, kinachovuta hisia za wengi ni uhusiano wake wa sasa, ambapo haijulikana kama yupo na Penny, Wema au wote kwa wakati mmoja!
Habari kwa msaada wa  venancefuraha.blogsport.com
  Usisahau kulike and share pia unatupata facebook .  swahili movies .com
pia follow us instagram  swahilimovies