All posts by swahili movies.com

BONGO MOVIES KUFANYA MAANDAMANO

 Wasanii wa filamu nchini Tanzania  wanaojulikana kwa jina la Bongo movies  wakati wakifikiria kurudi kwenye michezo ya tamthilia wameamua kufanya maandano katika mkoa wa dar es salaam siku ya Jumatatu tarehe 23 mwezi huu.

1Baadhi ya wasanii wa Bongo Movies

Akizungumza kwa niaba ya wasanii wenzake Issa Musa almaarufu kama Cloud amesema lengo la maandamano hayo ni kutokana na kuchoka na  wizi wa kazi zao za kisanii na kutaka   serikali isikie kilio chao na kutoa sheria kali kwa wale wote watakaobainika kuiba kazi zao .wakati huo huo jeshi la polisi kanda ya Dar es salam, Tanzania tayari imeisha toa kibali cha maandamano hayo.

imagesMr cloud

Swahili movies inawatakia maandamo mema na yenye kuzaa matunda .

Usisahau kulike and share pia unatupata facebook    swahili movies .com
pia unaweza follow us on instagram. swahilimovies

HATUJALALA NA MR NICE NI FILM TU: SOLANGE MSABAHA

Star wa movie nchini denmark awajia juu mashabiki wake wasiotaka kuelewa movie waliocheza na Mr nice.

      1231671_713164888700283_1079484579_nSolange Msabaha akiwa na uzuni

Hali hii za utata ilitokea baada za blog hii kuandika baadhi za part aliyocheya Mr nice na warembo hao wa v.a.d . habari hiyo iliyokuwa na kichwa cha habari , warembo wa vad wachanganywa na penzi la Mr nice . Ndipo hapo utata ulipoanzia

426416_600996803262374_1414397664_nTatu Daniel

Mashabiki wa kundi hilo la v.a.d linalokuja juu na  lililojipatia umaarufu Mkubwa nchini denmark   na nchi nyingi za ulaya na kote duniani kwa filamu nyingi zenye  utamaduni wa kiafrika pamoja na kukuza kiswahili na filamu kama   , Mistreated girl, Moyo Wangu , Tanzania to Denmark 1 , If i knew ,Dont look down to the poor  , na nyingine nyingi tu .

1391615_534162466672873_644130481_nDevotha Alfred akiwa kwenye pozi

Mashabiki hao Walikuja juu na kuanza kuwatukana warembo hao kuwa kitendo walichofanya cha kumpapatikia mwanamuziki mkubwa waliekuwa wakiigiza nae si kitendo kizuri bila kujua ile ilikuwa ni FILAMU tu na hakuna ukweli ndani yake ,

1523644_1400629200181055_881552633_oVumi Vane akiwa location

Lakini mastar hao hawakuonekana kujali sana  kutokana kuwa hakuna ukweli ,lakini kadri siku zilivyosonga ndipo mashabiki hao walizidi kushambulia kurasa za FACEBOOK za mastar hao wa v.a.d na kuwafanya wakose tena amani ndipo msanii Solange Msabaha alipowatolea uvivu na kuwajia juu kuwa wao ni wasanii na kazi wanayofanya ni kuelimisha  hivyo kilichoandikwa kwenye blog hii mara ya kwanza ni hadithi tu ya kwenye Filamu waliocheza na Mr nice na si vinginevyo .  Pata machache kutoka kwa msanii Solange  Msabaha

HABARI YAKO

Sio nzuri hata kidogo

TATIZO NI NINI MBONA UNANITISHA

Nilipenda kuongelea kuusu filamu iyi mpya tuliyo cheza na Mr Nice kwasababu watu wengi wanaongea kwamba  mimi Solange Msabaha , Devotha alfred,Vumi vane na Tatu Daniel tulifanya mapenzi yakweli na Mr Nice wakati sikweli, nilipata Message nyingi Sana watu wananiuliza kwa nini sisi tumejidhalilisha kwa kufanya mapenzi na Mr Nice wakati si kweli . Kwaiyo napenda watu wajue kwamba ni filamu tu narudia  tena na tena HATUJAFANYA MAPENZI NA Mr nice   .   kwasababu kuna jamaa mmoja alikuwa akinisisitiliza kwamba nikweli maana aliona picha  ambazo tulikuwa location tunashuti ,kama ambayo mimi na  Mr Nice tukiwa jikoni twapika ugali sasa jamaa kafikiria eti nikweli kabisa kumbe ilikuwa tunashuti tu .

1504125_1401552413422067_1240811111_nVumi Vane akiwa na Mr nice kwa ajiri ya kushuti

 POLE SANA KWA MASWAHIBU HAYO

Asante ila  bado sijapoa maana hawa watu hawataki kabisa kuelewa kuwa sisi ni wasanii tu na kila kitu tunachokifanya ni kuigiza kwa lengo la kufundisha , maana sisi wengine tumeolewa na tuna familia zetu  na tunamueshimu Mr nice kama msanii mwenzetu na kama kaka yetu,  na ndugu zetu na tunawaeshimu sana na wao wanatueshimu sasa wanavyosikia mambo kama haya wanajisikia vibaya kabisa .1476365_778923798791058_435752319_nSolange akiwa na Mr nice wanashuti movie Location

Sababu tu wao wanavyokazania kuwa sisi tumelala kweli na mr nice kwa kweli nashindwa kuwaelewa .na  naona  mtu kuwa msanii kunatokea  vitu vingi na kwasasa naona kuwa msanii ni vita vikubwa Sana kwa sababu inaomba mtu awe mvumilivu  Sana1486595_743010015727718_1778987873_nTatu akiwa na Mr nice wakishuti movie

swahili movies inawapa pole sana wasanii wa v.a.d kwa maswahibu hayo walikutana nayo kutoka kwa mashabiki wao ,nashukuru sana solange kwa ushirikiano wako na nawatakia kazi njema ya kuelimisha jamii na kutangaza lugha yetu ya kiafrika.

Usisahau kulike and share pia unatupata facebook    swahili movies .com
pia unaweza follow us on instagram. swahilimovies