Berlin Ujerumani hapatoshi MPOKI ndani ya nyumba soma hapa

 

MP Mfundo Mwenyekiti UTU_04
Mwenyekiti wa UTU Mfundo  Peter Mfundo Berlin, Ujerumani

Msanii maarufu nchini Tanzania  Kutoka kundi la Orijino Komedi al maarufu kama Mpoki (a k a Muarabu wa Dubai) anatarajiwa kuondoka nchini mapema mwanzo wa wiki hii kuenda nchini Ujerumani kwa ajili ya kuhudhuria  Mkutano mkuu wa Umoja wa Watanzania Ujerumani (U T U), utakaoambatana na Kongamano la kibiashara pamoja na Sherehe za Muungano wa Tanzania , zitakazoanza  siku ya ijumaa tarehe 25.04.14 na kumalizika siku ya Jumamosi Tarehe 26.04.14.  kuanzia saa 7 mchana katika ukumbi wa Deutsche Bank, Unter den Linden 13-15, 10117 Berlin, Ujerumani.
Akiongea na vyanzo vyetu vya habari msanii huyo alisema kuna umuhimu mkubwa wa safari yake ni  kuwakilisha wasanii wa Tanzania katika Tamasha hili kubwa  la aina yake, aidha aliendelea  kufafanua  kuwa wakati umefika kwa wasanii wa Tanzania kushirikiana kikamilifu na Watanzania wanaoishi nje ya nchi ili kuweza kupata fursa mbali mbali  zilizopo nje ya Tanzania, aliendelea kwa kusema  amevutiwa sana na Umoja Wa Watanzania Ujerumani (U T U) kwa shughuli zake   mbali mbali ambazo umekwishazifanya nchini humo  na ameamua kutoa mchango wake wa hali na mali kuhakikisha     (U T U) inafanya vizuri zaidi katika shughuli  zake mbali mbali. Ameongeza kwamba yeye binafsi amekuwa ni mfuatiliaji wa karibu sana  wa shughuli za umoja huo.
LOGO_UTU
Akiongea na vyanzo vyetu vya habari Mwenyekiti  wa Umoja Wa Watanzania Ujerumani U T U Bw. Mfundo Peter Mfundo alithibitisha kwa safari ya msanii huyo Maarufu nchini Tanzania. Alisema U T U Ilipendelea sana wasanii zaidi kuhudhuria sherehe hizi lakini kwa bahati mbaya  haikuwezekana  kutokana na mambo yalio nje ya uwezo wa  U T U, aidha  U T U  ni chombo kinachokubali sana na kuzifagilia kazi za wasanii wa Tanzania.
Mwenyekiti wa umoja huo anawaalika watanzania wote na waafrika katika sherehe hizo bila kukosa

 

 

IMG_2048Mpoki

 

Follow us on instagram swahili movies and Like our facebook pages Swahili movies.com and  for more updates about Swahili movies latest news, Scandal, Celebrities, features,european news, American,Australian ,Africa news, Music , news and more