Category Archives: NEWS

MAMA :UMAARUFU WA MOBETO NILIUONA MAPEMA


MAMA wa mwanamitindo mwenye jina kubwa Bongo, Hamisa Mobeto, Shufaa Rutiginga ‘Mama Mobeto’, ameibuka na kusema kuwa aliuona umaarufu wa mwanaye mapema tangu alipokuwa na umri mdogo. Akizungumza na Risasi Jumamosi, mama huyo alisema kuwa, mwanaye alionesha mapema atakuwa mtu f’lani kutokana na jinsi alivyokuwa akijiweka na watu wengi walimwambia kuwa atakuwa mlimbwende. “Unajua Mobeto alikuwa akijipenda tangu mdogo na alikuwa na mambo f’lani ambayo niliamini akikua atakuwa mtu f’lani mwenye jina mjini,” alisema mama Mobeto.
Mama huyo aliendelea kusema kuwa, baada ya kuona umaarufu wa mwanaye alijitahidi kumpa malezi mazuri na makini kwani alimlea peke yake bila kuwa na baba. “Baba wa Mobeto (Hassan Mobeto) alifariki dunia mapema sana hivyo nilimlea peke yangu na ni mwanangu wa pekee, nashukuru kuona anakua vizuri,” alisema mama Mobeto
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxBABA KANUMBA AIBUA MAPYA KWA waziri MWAKYEMBE


BABA wa aliyekuwa msanii maarufu wa filamu Bongo, marehemu Steven Kanumba, Charles Kanumba ameibua mapya kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Harrison Mwakyembe baada ya kumwangukia na kumuomba asimsahau katika mikataba aliyosaini mwanaye.

Akizungumza kwa njia ya simu akiwa nyumbani kwake Shinyanga, baba Kanumba alisema anamuomba waziri huyo amsaidie ili aweze kupata haki yake kama mzazi endapo mikataba ya kazi aliyoingia mwanaye enzi za uhai wake itafanikiwa.

Aliendelea kusema kwamba anaiomba serikali iingilie kati suala hilo na endapo fedha hizo za mikataba ya Kanumba zitatoka basi wasaini wote yeye na mama Kanumba na siyo waangalie upande mmoja yaani mama tu.

Namuomba sana Mwakyembe anikumbuke na mimi kwenye kusaini fedha za mikataba ya mwanangu iwapo zitatoka kwani nami nina haki maana nilimlea sana akiwa mdogo mpaka akawa mkubwa nikamuuliza anachagua kukaa wapi ndipo akachagua kwenda kuishi kwa mjomba wake. “Kwa sasa mimi nimekuwa mlemavu wa miguu hivyo naomba na mimi nikumbukwe, na mimi nina haki msinisahau,” alisema baba Kanumba.

Baba Kanumba ameya-zungumza yote hayo ikiwa ni baada ya hivi karibuni Waziri Mwakyembe kuzungumza bungeni kwamba watashughulikia mikataba ya kazi waliyoingia wasanii kama Mzee Majuto na Kanumba ili waweze kupata haki zao

STORI: Gladness Mallya, Risasi Mchanganyiko

xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx