Category Archives: fun

Umojaradio Uholanzi wakishirikiana na Ac Company-Ltd Uvira wanakuleta filamu bandika bandua

Umojaradio Uholanzi wakishirikiana na Ac Company-Ltd Uvira wanakuleta filamu bandika bandua ,na wamewataka mashabiki wao wote wakae mkao wa kula kwani kazi nyingi zinakuja umoja radio wameandika haya chini

Wadau wote wanaopenda maendeleo ya vijana wetu kutoka Jamhuri ya Kidemokratia ya Kongo, tumewaletea habari nzuri. Movie za AC Ac Company-Ltd Uvira zitakuwa hewani kwa mda wowote kwenye account ya Youtube ya umojaradio ” UmojaRadio NGG” waweza ku Subscribe ili wakati tutakapo weka au upload video hizi uwe wakwanza kupata msg ili kutazama uondo uhu wa vijana hawa ili kuwa sapoti kazi yao. Unakaribishwa ku share kwa wengine. LINK YOUTBE:
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
https://www.youtube.com/watch?v=EZ1h_PlCBnQ&feature=share


HURUMA :Baba OMMY DIMPOZI ADAI KATELEKEZWA NA MWANAE

Pichani mwenye tshet nyekundu ni baba yake mzazi Ommy Dimpoz ambapo Amesema mwanae huyo amemtelekeza miaka Mingi licha ya Dimpoz kusifika kwa kula bata nchi mbalimbali duniani. Baba Dimpoz Ana miaka 64 na ni dereva wa bajaji huko Tabora. Babaji amenunua mwenyewe. Wanaomjua wamesema anashindia mihogo na kachumbari !!

Mzee Faraji Nyembo akizungumza na Globalpublishers anasema

“Ni kama Wema Sepetu anavyohangaika kutafuta mtoto, siku akimpata hata kama hamsaidii chochote atamshukuru tu Mungu hivyo na mimi huwa ninamshukuru Mungu maana nimeshamleta Omary duniani. Yeye kama mtoto, ndiye anayetakiwa kujua mzazi wake anahitaji nini, yaani ukimuuliza sasa hivi Dimpoz akupe namba yangu, utaona, atakujibu nini maana ninaamini hana. Nimekuwa nikimpigia, lakini simu yake unaambiwa inatumika, angekuwa anaona umuhimu si angekuwa na namba maalum kwa ajili ya kuwasiliana na mimi baba yake kama mastaa wengine wanavyofanya kuwa na namba kwa ajili ya mashabiki na nyingine ya watu muhimu,” alisema na kuongeza

“Mfano nikifa kama leo ni bora huyo Ommy asinizike au kuja Tabora maana watu watampiga na kwanza atasema ni nani wake amefariki dunia maana hivi niko hai hana ushikiano,” alisema baba huyo.

Ommy Dimpoz ambaye amelelewa upande wa mama yake alipotafutwa na GPL hakujibu kitu kuhusu madai ya Baba yake huyo

CREDIT :TRIM SALEEM ;GLOBALPUBLISHER

XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX