Muigizaji Mrembo na chipukizi aamua kulikacha shavu la modeling kwenye kampuni kubwa ya kijerumani na kuingia kwenye utangazaji. Mrembo huyo mwenye mashiko na aliye serious na kazi yake ya uigizaji tulipomuhoji kuusiana na sababu gani za kuukacha uanamitindo ilihali yeye ni msanii na ana sifa zote za kufanya vizuri kwenye fani hiyo ya mitindo alikuwa na haya ya kusema.
Actress and TV host Devotha Alfred
Ni kweli nilipata kazi ya kufanya modeling kwenye kampuni kubwa hapa ujerumani inayofanya kazi na wanamitindo wa kiafrica , lakini nilikataa kuingia kwenye fani hiyo kwa sababu zangu binafsi ,ila kubwa kabisa ni muda kwa sasa nina programu nyingi ambazo zote zinaniitaji mimi niivest muda mwingi kuzishughulikia ikiwa kwa sasa nimechukuliwa na kampuni ya Afrowood ambayo ninawafanyia television show kwa lugha ya kiswahili japo show ina jina langu yaani DEVOTHA SHOW,
Lakini pia kwenye mambo yangu ya filamu mimi bado mchanga sana hivyo bado nina kazi kubwa ya kufanya kuinua sanaa yangu ikiwa pamoja na kuitangaza zaidi, kwa kufanya kazi nyingi nzuri na za kimataifa ,lengo langu kubwa ni kufanya kazi zenye ubora
Pia mimi ni mwanafunzi hapa ujerumani hivyo pamoja na shughui zangu zote za kilasiku bado shule inaniitaji nifanye vizuri ili nifikie malengo yangu, sasa najikuta muda wangu mwingi uko covered sina mda wa ziada wa kuingia kwenye mitindo kwani mitindo nayo ni kazi inayoitaji muda na kujitoa , ila kwa waafrica wanaoishi ulaya na hasa germany , kama wanajua wana vigezo vya kufanya kazi hiyo kimataifa basi hapo chini nitaweka contact ya hiyo kampuni ili mrembo ambaye yuko interested atawasilina nao wajue watamsaidia vipi kutimiza ndoto zake .
Tulipouliza devotha kuwa hizo ndio sababu za kukataa kazi hiyo hiyo kwa sababu za kimaadili au mavazi alikuwa na haya ya kusema
“hhahhahhahah kiasi sana si kweli sana kuwa nimekataa kwa sababu ya maadili maana kila kazi ina maadili yake na naheshimu kazi hii ya mitindo kwani kuna watu wanafanyakazi hii na bado wana image nzuri kwenye jamiii, ila kwa mimi tayari ni mtangazaji sasa tayari nimeshafunikwa na maadili mengine hivyo kuniwia ugumu sana kuingia kwenye mitindo kwani itaniweka kwenye sehemu ambayo mashabiki na jamii itashindwa sana kunielewa nasimamia wapi nafikiri hizi kazi mbili nilizonazo zinatosha kwa sasa asante.
https://www.youtube.com/watch?v=LoBEoYLTxuo
BONYEZA HAPA KUOMBA KAZI YA MODELING GERMANY
http://www.afrikanische-models.de/