Star wa movie nchini denmark awajia juu mashabiki wake wasiotaka kuelewa movie waliocheza na Mr nice.
Solange Msabaha akiwa na uzuni
Hali hii za utata ilitokea baada za blog hii kuandika baadhi za part aliyocheya Mr nice na warembo hao wa v.a.d . habari hiyo iliyokuwa na kichwa cha habari , warembo wa vad wachanganywa na penzi la Mr nice . Ndipo hapo utata ulipoanzia
Mashabiki wa kundi hilo la v.a.d linalokuja juu na lililojipatia umaarufu Mkubwa nchini denmark na nchi nyingi za ulaya na kote duniani kwa filamu nyingi zenye utamaduni wa kiafrika pamoja na kukuza kiswahili na filamu kama , Mistreated girl, Moyo Wangu , Tanzania to Denmark 1 , If i knew ,Dont look down to the poor , na nyingine nyingi tu .
Devotha Alfred akiwa kwenye pozi
Mashabiki hao Walikuja juu na kuanza kuwatukana warembo hao kuwa kitendo walichofanya cha kumpapatikia mwanamuziki mkubwa waliekuwa wakiigiza nae si kitendo kizuri bila kujua ile ilikuwa ni FILAMU tu na hakuna ukweli ndani yake ,
Lakini mastar hao hawakuonekana kujali sana kutokana kuwa hakuna ukweli ,lakini kadri siku zilivyosonga ndipo mashabiki hao walizidi kushambulia kurasa za FACEBOOK za mastar hao wa v.a.d na kuwafanya wakose tena amani ndipo msanii Solange Msabaha alipowatolea uvivu na kuwajia juu kuwa wao ni wasanii na kazi wanayofanya ni kuelimisha hivyo kilichoandikwa kwenye blog hii mara ya kwanza ni hadithi tu ya kwenye Filamu waliocheza na Mr nice na si vinginevyo . Pata machache kutoka kwa msanii Solange Msabaha
HABARI YAKO
Sio nzuri hata kidogo
TATIZO NI NINI MBONA UNANITISHA
Nilipenda kuongelea kuusu filamu iyi mpya tuliyo cheza na Mr Nice kwasababu watu wengi wanaongea kwamba mimi Solange Msabaha , Devotha alfred,Vumi vane na Tatu Daniel tulifanya mapenzi yakweli na Mr Nice wakati sikweli, nilipata Message nyingi Sana watu wananiuliza kwa nini sisi tumejidhalilisha kwa kufanya mapenzi na Mr Nice wakati si kweli . Kwaiyo napenda watu wajue kwamba ni filamu tu narudia tena na tena HATUJAFANYA MAPENZI NA Mr nice . kwasababu kuna jamaa mmoja alikuwa akinisisitiliza kwamba nikweli maana aliona picha ambazo tulikuwa location tunashuti ,kama ambayo mimi na Mr Nice tukiwa jikoni twapika ugali sasa jamaa kafikiria eti nikweli kabisa kumbe ilikuwa tunashuti tu .
Vumi Vane akiwa na Mr nice kwa ajiri ya kushuti
POLE SANA KWA MASWAHIBU HAYO
Asante ila bado sijapoa maana hawa watu hawataki kabisa kuelewa kuwa sisi ni wasanii tu na kila kitu tunachokifanya ni kuigiza kwa lengo la kufundisha , maana sisi wengine tumeolewa na tuna familia zetu na tunamueshimu Mr nice kama msanii mwenzetu na kama kaka yetu, na ndugu zetu na tunawaeshimu sana na wao wanatueshimu sasa wanavyosikia mambo kama haya wanajisikia vibaya kabisa .Solange akiwa na Mr nice wanashuti movie Location
Sababu tu wao wanavyokazania kuwa sisi tumelala kweli na mr nice kwa kweli nashindwa kuwaelewa .na naona mtu kuwa msanii kunatokea vitu vingi na kwasasa naona kuwa msanii ni vita vikubwa Sana kwa sababu inaomba mtu awe mvumilivu SanaTatu akiwa na Mr nice wakishuti movie
swahili movies inawapa pole sana wasanii wa v.a.d kwa maswahibu hayo walikutana nayo kutoka kwa mashabiki wao ,nashukuru sana solange kwa ushirikiano wako na nawatakia kazi njema ya kuelimisha jamii na kutangaza lugha yetu ya kiafrika.
Usisahau kulike and share pia unatupata facebook swahili movies .com
pia unaweza follow us on instagram. swahilimovies