Category Archives: Movies

Nafurahia kuwa single by Abou Hermis Twaleb

JINA LAKO HALISI NI NANI

Abou Hermis Twaleb    , Nimezoea kuitwa TWALEB…

1491329_390558261089385_838402233_oTwaleb

ASANTE ILIKUAJE UKAINGIA KWENYE SANAA TENA YA MAIGIZO, WHY NOT DANCING OR MUSIC.

 Tangu nikiwa mtoto ilitokea wazazi wangu wakagungua kuwa naweza Kuchora na kujiusisha sana na vitu kama Uigizaji nikiwa shuleni na hata kuwachekesha baadhi ya wana familia tunapokuwa nyumbani..Ndipo pale walipokigundua kipaji changu na kunipa moyo kuwa ni lazima nije kuwa msanii..ilianzia hapo

Swali lako kuhusu Why Not Music or Dance…Najisikia furaha sana kwa kuwa ,ukweli zaidi ni huu..Niliwahi hata kuwa Mshindi wa pili, Katika mashindano ya Disco mjini Tanga – Tanzania pale TWIGA HOTEL..na kuimba ni uamuzi tu kwa kuwa kitu muziki ndio ilikuwa Ndoto yangu kabla ya hata hamu ya kuwa Msanii au Actor kunipata..

KWA HIYO WEWE NI DISCO DANCER MZURI SANA.

Sana na wengi wanalijua hilo…Marafiki zangu wote walidhani ningeishia kuwa mwanamuziki..

SASA ULIINGIA RASMI LINI KWENYE SHUGHULI ZA FILM

Nilianza uigizaji pale RUSSIAN CULTURAL CENTER..nikiwa pamoja na watu kama Monalisa (Vyonne Cherry na mama yake Natasha, Tyson aliyetoka Kenya ambaye baadaye alioana na Monalisa..pia walikuwepo wasanii wengine wengi akiwemo RAY KIGOSI…… na baadaye Nilipata Nafasi ya kucheza SHORT film niliwa na Monaliza kama Girlfriend wangu ..wengine walioshiriki walikuwa ni Natasha  .mara tu nikaja Europe kutafuta maisha.  Pale Russian Cultural ilikuwa ni mazoezi tu tukiwa chini ya Mzungu mmoja .   Tyson wa Monalisa wakati huo alikuwa ndio kama kiongozi wetu kimazoezi.   na tukimaliza mazoezi tulikuwa tunakusanyika kutazama movie za wa-Nigeria

1508261_392687424209802_1570422092_nTwaleb

HONGERA ,UNA KIPAJI GANI KINGINE

Kwa upange wa Kipaji changu kingine cha kuchora au  Design  . Nilikuwa ni mimi kama mimi ninayeDesign cover za Cassatte karibuni dar nzima. nasema hivi kwa kuwa Maduka makubwa ya wahingi kama , Congo Corridor, Wananchi store, Mamu Store, Galaxy Music na mengineo Ni mimitu ndie niliyekuwa DESIGNER WAO….na wakati huo hakukuwa na CD wala DVD Tanzania…Kazi zangu hizi zote zilikuwa na jina “Artwork done by TWALEB” ..Namshukuru mungu kwa kipaji changu na nakumbuka wasanii wa zamani ambao niliwahi kuwatengenezea COVER zao ni pamoja na : Twanga Pepeta. FM Accademia, Hamza Kalala, Moshi William, na wengine wengi tu…

EH NIAMBIE SASA KUUSU TWALEB ENTERTAINMENT

Twaleb Entertainment Ni production yangu na namshukuru Allah kwa kuniwezesha kuitimia ndoto yangu hii. Nilipenda sana kumiliki Production mwenyewe kwa kuwa inanipa uhuru wa kufanya kila nipendalo. Production hii ilianza kama mwaka uliopita ingawa tayari nilishaanza kununua vivaa vya kazi miaka mitatu iliopita kidogokigodo.

Kuhusu ni kazi ngapi zilizofanya…ukweli ni kwamba ndio kazi ya kwanza iko jikoni katika hatua za mwisho na ni MOVIE yangu ya kwanza nikiwa kama Mmiliki wa production, Actor, Director na hata ukiniita Producer hutakosea. MOVIE hii inaitwa  AFRICAN BOY..Movie hii ni ya kiswahili na Subtittle ya Kingereza…nilitarajia ingekuwa tayari sasa..lakini kulikuwa na vitu muhimu sana vya kuweka sawa…hivyo kujipange kuipokea mwishoni mwa January..au mwanzoni mwa Feb na  hata Story na Script ni mimi mwenyewe.

1491221_392681054210439_387484194_nLucy K omba,Twaleb , Rachel  ndani ya African Boy1533437_392682537543624_1949734859_nTwaleb na Lucy Komba behind the scene AFRICAN  BOY MOVIE

HONGERA SANA KWA HILO NIMEONA UNATAFUTA VIPAJI  NA WATU WENGI WALIOJITOKEZA WAKO AFRIKA UTAWASAIDIA VP HAPO SASA.

 Kumekuwa na ugumu mkubwa sana ama tatizo kubwa kwa wasanii walio wengi sana kukosa wa kuwashika mkono na kuwaonesha njia…na wengine wamefikia kukata tamaa kwa kukosa wa kuwasaidia. Naweza kusema kuwa sitoweza kuwasaidia wote au kila mtu anayetaka msaada huo…hapana ila lengo langu ni kuwasaidia kwa kufanya nao kazi bila masharti yoyote..na endapo wanaweza kuendeleza vipaji vyao hivyo kwa kuheshimu utaratibu wa kazi..tutakuwa pamoja siku zote. Napenda niweke wazi kwamba wao wanaohitaji msaada huo wa kuinuliwa kwa vipaji vyao nao pia wajitahidi kunifikia kimawasiliano na waoneshe dhahiri kuwa wangependa iwe hivyo…nilitegemea hata hapa Denmark watakuja na kuitumia nafasi hii..lakini wengi wanaoonyesha nia hii wako mbali sana na TWALEB ENTERTAINMENT..

 1488376_392680177543860_1337312388_nTwaleb akiwa na Lucy Komba

TUONGELEE SASA KUUSU UMOJA ,UMEANZISHA UMOJA UNAITWA  S.A.F.U kitu gani kimekusukuma

Nia yangu ni tukukutanisha kiusanii na kujaribu kudumisha umoja na upendo kati yetu, na kikubwa zaidi ni kukuza KISWAHILI na kuwaweka Waafrika wanaoishi maeneo ya huku wawe karibu zaidi kiusanii . Umoja ni kitu kizuri sana kwa kuwa sisi binaadamu tuko tofauti na pia tuna mawazo tofauti sana..hivyo ipo haya ya kubadilishana mawazo kwa njia hio ya kuwa na Umoja..

JE UMEOA TUAMBIE KUUSU MAISHA YAKO KWA KIFUPI.

Swali lako zuri ..lakini ningefurahi kulijubu kwa kifupi sana…KWA SASA NIPO SINGLE…..  lakini Nafurahia sana USINGLE wangu…

912520_392687224209822_978678843_nTwaleb

CHANGAMOTO GANI UNAZIPATA KWENYE KAZI YAKO

 Changamoto zipo na ni nyingi sana..na si tu kwa sisi tunaoingia sasa kwenye Industry hii.  hata Wasanii wakubwa wote wana kutana na Changamoto tena kubwa zaidi…Sina kikubwa cha kukwambia ila ni Furaha yangu tu ya kuweza kufikia hapa  kwa uwezo wa ALLAH na niko na mipango mingi ambayo nisingependa kuiweka wazi kwa sababu zangu za kimsingi ila..ninafurahi kila pale ninapoona Fanz wangu wako wengi na wanazidi kunisupport  kwa kuwa bila wao sitafika popote.   kunifanya nijisikie raha sana kwa kuwa bila wao sitafika popote..

Swahili movies  inashukuru sana Abou Hermis Twaleb kwa ushirikiano wako.. tunakutakia kazi njema ,pata habari zaidi tembelea  facebook page yetu swahili movies .com

 

Natafuta mtu mwenye kipaji cha kuongea: Rehema Nkalami

JINA KAMILI UNAITWA NANI
Naitwa Rehema Amiry Nkalami natokea Tanga Tanzania .Ila naishi silkeborg Denmark  ni mtangazaji wa swahili talk radio.

http://www.shoutcast.com/Internet-Radio/swahili%20talk%20radio

401299_168329066660613_904520870_nRehema Nkalami akiwa Studio

Hongera sana kwa kazi yako nzuri ya utangazaji, sasa ningependa kufahamu hii kazi ulianza lini
Asante sana , hii kazi ya utangazaji niliianza mwaka 2012  . sifanyi hii kazi sababu  napenda utangazaji tu ,hapana bali napenda kuutangaza Uafrika pamoja na lengo la kukuza lugha za kiswahili na utamaduni wa mwafrika ulaya na nchi zote ulimwenguni.

1374284_222645964562256_317310790_n

Rehema akiwa na kikundi cha African Umoja Denmark kwenye sherehe ya utamaduni

577440_227389214087931_2133106632_nRehema akitangaza mavazi ya kiafrica kwenye Swahili talk radio

Unaweza vipi kufanya hii kazi ukizingatia wewe upo ugenini
Siku zote mtu anayenitia nguvu ni mme wangu mpendwa Søren . Yeye ni muandishi wa habari pia ni mtangazaji wa denish radio station,
lakini pia mimi nina studio yangu hapa silkeborg na zaidi nafanya kazi na jamii ya waafrica, pia watu wote ambao wanapenda kuongelea mambo yanayohusu Africa wanakaribishwa studio.

577577_170101323150054_825325804_nRehema akiwa studio na Leonidas  kwenye kipindi cha biblia1471962_241447069348812_1335462501_nRehema akimuhoji Mr Nice mwanamziki  kutoka Tanzania

Hongera sana kwa kazi zako nzuri, sasa ningependa kujua mipango yako ya baadae.
Mipango yangu ni kuanzisha Tv talk show ambayo itaitwa REHEMA SHOW na kwa sasa maandalizi yote yameshakamilika  ,niko kwenye hatua za mwisho ili kuanza kazi hiyo, na sababu mimi nitakuwa busy na talk show hivyo natafuta msaidizi kwenye radio mwezi wa pili ,mtu mwenye kipaji cha kuongea hasa kipindi cha kuchekesha

1482156_10202894906313386_1034128203_nRehema akiwa na Lucy Komba muigizaji toka Tanzania

1472036_241447519348767_989828999_n

Rehema akimuoji Raisi wa v.a.d film production Mr Safari Lukeka

Hongera sana dada Rehema kwa kazi nzuri unazozifanya ikiwa si tu kwa utangazaji bali hata kuutangaza uafrika pia kushughulika na mambo yanayousu jamii ya waafrica , Swahili movies inakupongeza na kushukuru kwa ushirikiano wako .

Usisahau kulike and share faceboook page yetu swahili movies .com