Mtangazaji na Muigizaji wa VAD film production Devotha ashindwa kumalizia kushuti baada ya lens feki moja aliyoweka jichoni kuanza kumsumbua na kukataa kutoka, kititim hicho kilitokea wakati mwanadada huyo akiwa nchini Denmark wakati wa kumalizia filamu yake ,
MSIKILIZE MWENYEWE HAPA
Hii sio mara ya kwanza mara nyingi navaaga hizi eyes contact lakini mara ya mwisho nilipokuwa Copenhagen narekodi show yangu niliivua lens moja na kusahau kuirudisha kwenye maji yake maalumu , baada ya mda nilipokumbuka ndipo nikawai kuirudisha lakini naona ilikuwa imearibika bila mimi kujua.
Nilipofika mji mwingine baada ya kushuti ndipo kuna scene nilipendelea tena nivae eyes contact lakini hali ikawa tofauti ile lens niliyoisahau kuiweka ikaanza kuuma jicho la kushoto likaanza . nikaona bora niitoe ili iwe sawa lakini wapi ikaanza kukataa hata kutoka hapo sasa wasanii wenzangu kweli walishangaa na hata kuanza kuogopa kuniangalia jicho hilo kwani lilianza kutisha na kuwa jekundu sana .
mwisho wa siku nikashindwa kutoa na kwakuwa nilikuwa ugenini nikaona nirudi haraka Germany ili hali ikiwa mbaya niende hospitali nitolewe nashukuru Mungu asubui ikatoka lakini jicho likawa bado linauma sana sana na hata kuangalia mwanga nikawa siwezi tena , nikavaa miwani mweusi lakini bado , Aisee hivi vitu vya bandia tuwe navyo makini sana wasanii wenzangu maana unaweza mtu kupofuka ukubwani hivihivi.Devotha akiwa na eyes contact za blue
Devotha akiuguliaLens baada ya kukubali kutoka jicho la kushoto
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
BONYEZA HAPA KUPATA SHOW YA KIJANJA NA KUJUA MAISHA HALISI YA ULAYA
https://www.youtube.com/watch?v=K1BsICrQ6GU