Frank Amshushia Lawama Riyama kwa Kumzibia Riziki.

 

RIYAMA887

Mwigizaji  mkongwe wa filamu za hapa Bongo, Mohammed Mwikongi maarufu kama Frank, amedai kuwa mwigizaji mwenzie Riyama Ally anamzibia riziki kiasi kwamba sasa anamsaka ili amweleze kitu gani aliwahi kumkosea.

Akizungumza jijini hivi karibuni, Frank alisema anamtafuta Riyama ili aweze kumwambia ni kwa nini inakuwa hivyo kwa sababu katika filamu zote ambazo yeye anatakiwa kucheza, mwenzake huyo huwepo na ndiye anayependekeza watu watakaohusika na filamu hiyo.

“Tukiacha ile filamu iliyofanyika nchini Uingereza ambayo iliandaliwa na Dida Entertainment, kuna filamu nyingine iliandaliwa na Mbunge Shamsa Mwangunga ambaye alinipigia simu na kuniomba nicheze nafasi aliyoipendekeza lakini baada ya siku, nafasi yangu ikachukuliwa na Slim.

“Pia kuna nyingine ambayo iliandaliwa na mtu wa mtaani kwetu ambaye ni mfuatiliaji mzuri wa kazi zetu, nafasi yangu ikachukuliwa tena na Msungu, sasa mimi namtafuta Riyama aniambie ni kwa nini huwa ananizibia riziki yangu wakati imeshapangwa,” alisema.

Riyama hakuweza kupatikana kupitia simu yake ya mkononi kwani mara zote iliita bila kupokelewa. Hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maneno haukujibiwa.

GPL

Follow us on instagram swahili movies and Like our facebook pages Swahili movies.com and  for more updates about Swahili movies latest news, Scandal, Celebrities, features,european news, American,Australian ,Africa news, Music , news and more

CREDIT :Bongo movies

Tupe maoni yako hapo Chini..!!