Hamisa Mobeto asema Zari atamuua mama yake kwa presha, akiri kuzidiwa nguvu na Team Zari

nbm

Kufuatia mtifuano wa beef lao Hamisa Mobeto asema Zari atamuua mama yake kwa presha, akiri kuzidiwa nguvu na Team Zari

“Yani kwa kweli Zari huyu atamuua mama yangu. Unajua nini, hawa watu wanaompigania Zari katika mitandao ya kijamii, kwa sasa wamefikia hatua mbaya sana. Wanamtukana sana mama yangu bila hata sababu za msingi. Yani kuna vitu vizito sana vinaandikwa hadi mama anapata mshtuko,” alisema Mobeto alipoulizwa na GPL

Mobeto aliweka wazi kuwa, endapo Zari angewasihi watu wake waache kumtukana mama yake, wangeweza kumtii lakini kwa sababu amekaa kimya, ndio maana wanapata kichwa.

Hata hivyo, rafiki wa karibu na Mobeto ambaye hakutaka jina lake liwekwe wazi, alimshauri mrembo huyo kufanya mambo matatu ya msingi ambayo yatamfanya awe salama, yeye pamoja na mama yake. Alisema….

1. “Aache kushindana na Zari. Yeye asifanye kitu kwa kushindana na Zari. Afanye kazi zake bila kuonesha kwamba anamtambia Zari au kutaka kushindana naye kwa namna yoyote. Si unakumbuka alivyoandaa shughuli ya arobaini ya mwanaye, yani aliweka zile mbwembwe za gharama ili mradi tu afikie levo za Zari kitu ambacho si sahihi. Alijikuta anaahirisha shughuli hiyo kwa kukosa fedha hadi pale alipofanikiwa ndio ikafanyika. We angalia shoo ya juzi kule Uganda, kakubali kwenda kufanya shoo siku moja na Zari bila kujua kule mwenzake ni kwao hivyo kujikuta akifunikwa bila sababu za msingi.”

2. “Ili awe salama, hapaswi kujibu wala kuanzisha kijembe chochote katika mitandao ya kijamii. Yeye aweke masuala yake yanayomhusu tu, aachane kabisa na Zari.”

3.“Akae mbali na mzazi mwenzake ambaye anaonekana kulalia kwa Zari. Ni dhahiri kwamba mwenzake ndiye kinara katika huu mvutano. Zari amekaa muda mrefu kwenye uhusiano kuliko yeye hivyo hawezi kumuacha kirahisi. Yeye angetafuta tu mwingine, akaendelea na maisha yake,” alimaliza kusema rafiki huyo wa Hamisa Mobeto. credit: GPL

Nini maoni yako ?

CREDIT ; TRIM SALEEM

XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX
Kufatilia maisha ya ughaibuni subscribe kwa vlogers hapa chini kuona video zao nyingi


https://www.youtube.com/watch?v=dr-43tMZd8kh