VAD likiwa na maana ya Voice Of Africa In Denmark ilianzishwa mwaka 2011 na inapokea msanii yeyote mwenye nia ya dhati katika kuitangaza Afrika kupitia sanaa ya filamu na mwenye kipaji cha uigizaji bila ubaguzi wowote.kabla ya kuukaribisha mwaka mpya nilipata muda mzuri wa kujua mawili matatu kutoka kwa kampuni ya V.A.D iliyovunja rekodi kwa mwaka 2013 kwa kazi nzuri za film nchini denmark na ulaya kwa ujumla kampuni lakini kabla ya kusema mipango yao ya 2041 tujikumbushe mambo mbalimbali ya 2013
WALINIKIWA KUMLETA NA KUFANYA KAZI NA MUIGIZAJI NYOTA KUTOKA TANZANIA .LUCY KOMBA MOVIE INAYOITWA TANZANIA TO DENMARK, Fuatilia picha chini
wasanii wa v.a.d wakiwa na lucy komba
wakishuti tanzania to denmark na lucy komba
wakishuti tanzania to denmark na lucy komba
VAD FILM PRODUCTIONS WALIFANIKIWA KUIINGIA MIKATABA YA FILAMU NA KAMPUNI ZA NORDISK FILMS NA BOLIG AALBORG, WAFUNGUA AKAUNTI MPYA YOU TUBE BAADA YA KUFANYIWA HUJUMA AKAUNTI YAO YA ZAMANI kuhusu maeneo ya location ya filamu watakazokuwa wanatengeneza na Bolig Aalborg ambalo ni shirika la nyumba la Nordjylland na picha hapo chini zinaonyesha wakati wasanii hao walipokutana na shirika hilo kuangalia nyumba zao mpya ambazo tayari wameshajenga na nyingine bado zinajengwa kwa ajili ya kutumia kama location wakati wa kutengeneza filamu.
WASANII WA V.A.D WALIWEZA KUSHIRIKI KATIKA TAMASHA KUBWALA FILM KUTOKA AFROWOOD FILM FESTIVAL 2013 NCHINI DENMARK.
Afrowood Film Festival kwa mara ya kwanza ilifanyika katika ukumbi wa Culture Centre, Copenhagen, nchini Denmark na kuwakutanisha wadau mbalimbali wa filamu. Na filamu za kiswahili ziliwakilishwa na wasanii kutoka VAD Production, Twaleb Entertainment. Wageni waalikwa kama vile Tanya Kersey kutoka Hollywood, Yvonne Hans(Uk/Nigeria), Obi Ikenna(Uk, Nigeria, Marie K. Gomez na wengineo walikuwepo na kufurahia kuziona filamu za kiswahili na za lugha nyingine . Wadau hao walibadilishana uzoefu na kujifunza zaidi kuhusu filamu.Angalia baadhi ya picha za matukio ya Afrowood…………..
wasanii wa vad siku zote ni watu wenye umoja hivyo pia walifanikiwa kushiriki harusi ya msanii mwenzao wa scandinavia
V.a.d. waliweza kumwalika na kucheza film na msanii maalufu kutoka Tanzania Mr nice
Mr Nice kutoka Tanzania ambaye ni msanii wa muziki wa kizazi kipya aliyewahi kujipatia umaarufu mkubwa ndani na nje ya nchi akiwa na style yake ya Takeu kupitia nyimbo kama Kidali Po na Kikulacho amepata nafasi ya kucheza filamu huko Denmark kupitia wasanii wa VAD productions wenye asili ya kiafrika
Sasa hayo ndio mambo ambayo v.a.d ilifanya ili kukufurahisha wewe shabiki wao wakuwa na watu tofauti kama Lucy Komba, Nordisk Film, Biligskab Aalborg, Afrowood Film Festival 20013 Copenhagen na Mr. Nice na kwa mwaka 2014 umependelea V.a.d ifanye nini? leta maoni yako hapo chini ili vad iendelee kukuburudisha …
Usisahau kulike and share pia unatupata facebook . swahili movies .com
pia follow us instagram swahilimovies