HIVI NDIVYO ALI KIBA ALIVYOMWAGIA SIFA DIAMOND

 

ali-kiba-na-diamond-667x515

Ni siku chache zimepita tangu tamasha la Serengeti Fiesta lifanyike, ambapo tulishuhudia baadhi ya wasanii wa hapa Bongo wakipata nafasi ya kushare stage na wasanii wakubwa wa Afrika kama Davido na Waje huku kutoka Marekani alikua ni msanii T.I.

Ni ukweli usiofichika kua Fista ya mwaka huu imekua gumzo kubwa hasa baada ya kutokea mzozani kuhusu nani mkali zaidi kati ya Ali Kiba. Japo kulikua hamna ushindani lakini mashabiki wa wasanii hawa wawili wamekua katika marumbano makali kuhusu alimfunika mwenzake.


Millard ayo kupitia Ayo Tv alipata nafasi ya kufanya mahojiano na Ali Kiba kuhusu wasanii waliofanya poa stejini na alikiba alianza kwa kusema ” Nilichelewa kufika sikuweza kuwaona kina Ommy Dimpoz, Vanessa na kina Young Killer lakini niliobahatika kuwaona wote wamefanya kazi nzuri, nilimkuta Waje na Panto walifanya vizuri japo ni nyimbo zao chache tunazijua ” akazidi kufunguka zaidi kwa kuwataja wasanii ambao anaona yeye walifanya vizuri ” Mr Blue amenifurahisha sana, WEUSI wamefanya kazi nzuri…. kina Diamond wamefanya kazi nzuri pamoja na Linah ”
Hii inaonyesha wazi kuwa kiba haitaji bifu na mtu ila anaangalia mziki wake ulipo na anapoelekee  kwan mara ya mwisho kufanya mahojiano na thesupestarstz ally kiba alisema anawashangaa watu wanaomfananisha na mtu mwingine huku akiongeza kiba atabaki kuwa kiba na wao wataendelea kuwa wao.

Follow us on instagram swahili movies and Like our facebook pages Swahili movies.com and  for more updates about Swahili movies latest news, Scandal, Celebrities, features,european news, American,Australian ,Africa news, Music , news and more

CREDIT : HERE

Tupe maoni yako hapo Chini..!!