Huyu ndio Mdenish anayeimba kwa kiswahili fasaha msikilize akiimba na Dennie Njonanje

Msanii Dennie Njonanje akitoa Story na maudhui ya mwimbo wake, maelezo haya aliyotueleza alipokuwa akihojiwa na (SWTR- Swahili Talk Radio by Rehema Nkalami)

10171671_693357747369487_263497712960392615_n

Mwaka 2012 nilipokuwa Zanzibar katika chuo kiitwacho Dhow Countries Music Academy (DCMA) kwa lengo lakujiendeleza kimuziki, nilikutana na Andreas Nim na tukafanya Jam Session na kila mmoja wetu kuridhika na perfomance ya mwenzake. Tukaamua kutengeneza wimbo pamoja.Maudhui ya wimbo huu haswa ni mapenzi, namimi nimejaribu kumuongelea msichana kwa njia ya tofauti kidogo kuonyesha uzuri wa mwanamke hasa katika dunia ya leo ni kipi cha kuzingatia, na kwa mtazamo wangu yakinifu msichana bora ni yule anayejitambua, mchapakazi na anayefahamu umuhimu wake katika jamii.

Baada ya recording, ilibidi kufanya video na lakini director ambaye tulimuamini zaidi Amit Raja alipata udhuru na hivyo hatukupata nafasi. Na hii ndiyo sababu iliyochelewesha hata audi hii kufika kwenye vyombo vya habari. Tutafanya punde tupatapo nafasi kwasababu sasa na mimi nipo Ujerumani na siyo mbali sana na Denmark anapoishi Andreas.

Mapokezi na single yako, na Mdenish alie shiriki kwenye single yako, je amepokeaje lugha ya Kiswahili?

Mapokezi ya muziki wangu kwa kawaida huwa ni mazuri. Kwakawaida najitahidi kuandika tungo zinazoburudisha, kufundisha au kuhamasisha pasipo KUDHALILISHA jinsia fulani. Andreas ni mtu ambaye anapenda sana kujifunza kitu kipya hivyo alifurahia sana wimbo huu na bado tuna ahadi ya kufanya kazi pamoja hapo baadaye.

Unawaeleza nini Wasaa wa Kiafrika waishio nje ya Afrika kuhusu kuimba kwa Lugha ya kiswahili?

Kiswahili ni lugha kubwa kuliko zote katika jamii ya Wabantu, pia moja kati ya lugha maarufu na yakimataifa kutoka Afrika. Hili ni jambo lakujivunia sana. Hivyo kwa msanii kutumia lugha ya Kiswahili ni mchango tosha wakuitangaza lugha na asili yake. Kama mimi nikiimba, mfano kwa kiingereza, na Justin Timberlake akaimba kiingereza ni nani utamsikiliza?

Kwanini hujaimba kwa kigerman?

Sikuwa, na wala sina sababu yoyote ya kuimba kwa kijerumani kwasasa japo baadaye nitafanya hivyo kama kuongeza vionjo tu. Ninapotumia Kiswahili huwa nina uwanja mpana sana wa kuelezea hisia zangu na mawazo yangu kwa hadhira kuliko nitumiapo lugha ngeni. Nawatakia Kazi njema na shukrani za dhati kwa kusapoti wasanii tunaoishi ugenini.

Je unategegemea wa German kusikiliza mziki wako?

Kwa hapa Ujerumani ninao wapenzi wa muziki wangu na kila nifanyapo onyesho wengu hufarahi kwasababu wanapata ladha tofauti pia huwa nawajengea picha halisi ya Afrika ambayo wengi huisikia na kuiona katika vyombo vya habari. Dhumini langu kwa sasa ni kujitambulisha kwa Waswahili wenzangu waishio ughaibuni. Ninaandaa albamu ya mimi mwenyewe na natarajia kuizindua mapema mwakani. Baada ya hapo nitafanya matembezi ya kuitangaza ndani na nje ya Ujerumani. Itakuwa na nyimbo 12, kama vile NGUZO MAMA, JIONGEZE, HESHIMU KAZI na MAHABA YA KALE itakuwa ya mwisho kutoka kisha utambulisho wa album utafuta.

Naishukuru sana Swahili Talk Radio kwa ushirikiano wenu pia kwakuunga mkono kazi za waswahili.

Upendo, Amani na Umoja ndiyo nguzo zetu.

Follow us on instagram swahili movies and Like our facebook pages Swahili movies.com and  for more updates about Swahili movies latest news, Scandal, Celebrities, features,european news, American,Australian ,Africa news, Music , news and more

CREDIT :Swahili talk Radio

Tupe maoni yako hapo Chini..!!