Ifahamu Afrohoodstz Community Media Tanzania na kazi zake hapa

10403512_803289449716200_2348293451208005321_n

Tuambie kifupi kuhusu Afrohoodstz Community Media

Hii ni kampuni inayojihusisha na utengenezaji wa filamu , ambayo ilianzishwa Rasmi 1/3/2013 na mimi mwenyewe, msukumo wa kuanzisha kampuni hii ilitokana na changamoto nilizokuwa nikiziona baina ya wasanii wenzangu watanzania ambao tunafanyia sanaa yetu katika makundi .mara nyingi unakuta wasanii wapo katika makundi kwa zaidi ya miaka minne hadi mitano lakini hata siku moja hakuwahi kupata fursa ya kurekodi filamu…sababu ni gharama kubwa za kurekodi filamu ambazo kampuni chache zilizopo zinatoza.

Pia hata ukikuta wameweza kurekodi basi ubora wake ni tatizo, unakuta kila kitu kimefanyika katika ubora wa chini sana ambapo haitaweza kufanya vema sokoni.hapo ndipo nikaona kuna umuhimu wa kuanzisha hii kampuni ambayo itatoa fursa kwa nini kwa ajili ya kusaidia hizi changamoto ambapo zaidi nitafaanya kazi na vikundi vya wasanii wachanga kwa gharama ndogo, kwa ubora wa hali ya juu na malipo yatakuwa baada ya kazi kufanyika na kuuzwa.

10352943_1500348053515780_7983849906858581290_n

Namaanisha mtindo Wa post paid au mali kauli. Kwa maana hii kigezo kikubwa kuliko vyote ili uweze kufanya kazi na kampuni yetu ni ubora wa kazi yako ambao utatuhakikishia upatikanaji wa soko. Ndio maana hata jina likawa afro-hood-tz community-media…Kama chombo cha wanajamii wa afrika Ilianzaje Baaada ya kulifanyia utafiti wazo langu na nikaona kwamba linauzito,jambo la kwanza nilishirikisha familia yangu ili iweze kunipa baraka ya kutumia baadhi ya fedha tulizokuwa tunazipata katika kipato chetu cha kila siku kwa ajili ya ununuzi wa vifaa.Nashukuru mungu walinielewa na wakawa msukumo wa kuniuliza kila kukicha lini ningefanya, maana baada ya kupata wazo hili nilijikuta nimesimamisha harakati zote za kisanii ikiwepo ni pamoja na kutoshiriki filamu yoyote kwa kipindi chote kuanzia mwaka 2013…

nilianza kutunza fedha kwa ajili ya kununua kamera, na vifaa vingine, hadi kufikia january mwaka huu nilikuwa nimeshaweza kununu vifaa vya msingi kwa ajili ya kurekodia filamu…Lakini wakati huo nilipokuwa katika harakati za kutunza pesa kwa ajili ya vifaa nilianza kutengeneza timu , na hadi kufikia vifaa vinakamilika tayari nilishakuwa na timu ya muhariri (editor), muongozaji, (director) mwandishi(writer)cameraman na graphic designer ambao wote walikuwa na mtizamo wa kujiwezesha kujiajiri kulingana na vipaji vyetu. Viongizi Kulingana na uchanga wa kampuni, uongozi wa kudumu ni mwanzilish na mtendaji mkuu(Josephat J Mushi) ,muhasibu (Glory Josephat), mratibu /coordinator (Kadigiri David) Lakini huwa tuna uongozi wa muda mfupi katika kila mradi (project) kulingana na ukubwa wa mradi husika,

1978828_809732809071864_3355529783252178646_n

Na malengo yake Ukiachilia mbali lengo la msingi ambalo ni kujiajiri kwa vipaji, pia tunamalengo na mikakati ya kutufanya tufike kimataifa na kuwafikia vijana wengi zaidi hapa tanzania na nje ya tanzania.leo tumeanza kufanya filamu lakini bado tunamalengo makubwa ikiwa ni pamoja na kujenga Theatres kwa ajili ya wasanii kujifunza, kufungua vituo vya radio na television maalumu kwa ajili ya filamu na vipaji vinavyohusika na filamu. Malengo madogo madogo ni pamoja na kuandaa proffessional stage plays ili kuwapa fursa wasanii kupata ajira za kila siku.

Na wewe Kama kiongozi wa afrohood kituganni kilikuvutua kwenye filamu

Kabla sijawa msanii wa kuigiza, nilikuwa msanii wa muziki na maigizo kanisani wakati nina umri mdogo sana, lakini nilipojua kusoma na kuandika taratibu nikapata msukumo wa kuandika kitabu,na hadithi and I was the best on that. Nilipofika sekondari tayari nilikuwa ninamadaftari kadhaa ya story..ambazo nilizipenda zaidi ilikuwa ni “Love devil” na “its revenge not love” .baada ya kuandika hadithi hizi , nilikutana na jamaa mmoja ambaye alikuwa ni msanii na director wa kundi moja pale dodoma, nilimuonyesha stori ya “love devil” akavutiwa sana ,akaniambia ile ni story nzuri ya filamu…pia akaniambia muonekano wangu ungenifanya niwe mwigizaji mzuri, basi akaanza kuniandaa kuwa msanii, baada ya hapo nikakutana na madairekta wakubwa hapa tanzania nikapitia kwenye academy mbalimbali na kampuni hadi nimekuwa na kampuni leo hii.

1780677_712286402149839_1409986038_n

Mmeshafanya filamu ngapi na mnaonaje changamoto katika shughuli nzima za filamu

Kama kampuni tumeshafanya filamu mbili (2), ambayo moja ni filamu fupi ambayo imegharamiwa na mimi mwenyewe, inayoitwa JILINDE NA UWAPENDAO, ambayo ni filamu juu ya ugonjwa hatari wa UKIMWI, filamu nyingine inaitwa THE GREAT NAME. filamu ya wasanii wachanga waliopo kijiji cha Masumbwe ,wilaya ya kahama mkoa wa shinyanga. Ambayo kwa sasa ipo katika hatua za mwisho za uhariri.

10498460_809739705737841_5332176897082491642_o

Changamoto Ni zipi kitu gani unafikiri kiboreshwe mfike kimataifa

Changamoto ni nyingi sana, lakini zaidi ni mfumo wa soko la filamu la Tanzania ambao umekuwa ukikandamiza uwekezaji katika filamu. Ila pamoja na hilo ambalo tunalipata wasanii wote wa tanzania ambalo shirikisho la filamu (TAFF) wamekuwa mstari wa mbele kulisimamia hilo, lakini pia kampuni nimekuwa bado nikiiendesha kwa gharama zangu , bado haijaweza kujiendesha, lakini pia mahitaji yamekuwa yakiongezeka kila kukicha wasanii wamekuwa wakinifuata ili niwasaidie…technologia inakuwa kila leo hivyo kila kukicha nalazimika kuboresha vifaa mbali mbali. Je wewe una familia unapenda kutuambia kuusu familia au hapana….

Hahaha. Ndio mimi ninafamilia ya mke mmoja na mtoto mmoja wa kiume anaitwa Johnson Josephat ambao wamekuwa na msukumo chanya katika kampuni hii. Nawapenda sana na kila siku ninawashukuru kwa kuniwezesha kufika nilipo leo Unaishi wapi na offisi za afrohood ziko wapi Ninaishi Jijini Mwanza, na ofisi za afrohoodstz community media zipo Mkolani Jijini mwanza Kuna wasanii wengi wachanga mnawafikiriaje kuwainua Kampuni ina wataalamu wa filamu ambao huwasaidia wasanii wachanga katika techinical side,na ushauri, lakini pia kwa wale waliokaribu tunawashirikisha katika project kubwa za tunazotegemea kuzifanya chini ya kampuni, pia tunawatengenezea filamu kwa gharama nafuu sana na kwa mtindo wa mali kauli,kuwaelekeza sokoni na ushauri katika soko 980043_621367854623739_8675256289334949884_o

Tuambie kuusu filamu hii ya Jilinde Na Uwapendao Na changamoto itatoka lini Ni watu watarajie nini zaidi kutoka kwenu

Filamu ya jilinde na uwapendao imeshakamilika hadi sasa , hii ni filamu fupi ambayo kampuni imeitengeneza kama zawadi kwa mashabiki wake, ambayo inategemewa kuzinduliwa Rasmi 1/12/2014 ambayo ni siku ya Ukimwi Duniani hapa kanda ya ziwa, michakato tayari imekwisha anza , na tunaamini itakuwa event kubwa sana kwa kampuni yetu na wanajamii kwa ujumla maana Tatizo la ukimwi bado lipo na katika filamu hii tumeliangalia kwa mtizamo tofauti sana, lakini pia wasanii wameonyesha uwezo mkubwa sana …naomba nisiiongelee sana hii sababu ni mengi kuhusiana na hili.

906553_623407041086487_1709138794125904715_o

Lakini pia hapa mbeleni tuna project ya filamu ya MKONO MWINGINE ambayo ni filamu ndefu ya maisha, inayozungumzia mambo yaliyopo katika maisha ya mtanzania /muafrika wa leo,Tayari kampuni imeshafanya mawasiliano na msanii maarufu hapa tanzania Zuberi Muhamed (NIVA) na amekubali kufanya film hii,hivyo wapenzi wakae mkao wa kula… Lakini pia afrohoodstz inaushirikiano wa karibu na kampuni kubwa hapa Tanzania na nje ya nchi wanaofanya swahili movie, na zipo project zinazofanywa kwa ushirikiano na wadau wa filamu waliopo Denmark na Ujerumani, ikiwa ni pamoja na Tamthiliya , ila ni mapema kuzizungumzia hizi ntazitafutia wakati wake rasmi…

10355595_623381084422416_6853756016278714974_o

Follow us on instagram swahili movies and Like our facebook pages Swahili movies.com and  for more updates about Swahili movies latest news, Scandal, Celebrities, features,european news, American,Australian ,Africa news, Music , news and more

CREDIT :Here

Tupe maoni yako hapo Chini..!!