Kesi ya Wema; Wakili Apinga Ushahidi wa Mkemia Mkuu

KESI inayomkabili staa wa Bongo Muvi, Wema Sepetu, imeahirishwa hadi Agosti 4 mwaka huu ambapo Hakimu Mkazi, Thomas Simba, atatoa ufafanuzi juu ya taarifa iliyosomwa na ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali.

 

Kesi hiyo imeahirishwa kutokana na wakili wa utetezi, Peter Kibatala, kusema ripoti hiyo ina mapungufu mengi ya kisheria na hivyo hakimu akawaomba mawakili pande zote mbili kuridhia apate muda wa kuipitia ili itakapoendelea aweze kuitolea ufafanuzi.

 

Awali, kesi hiyo iliahirishwa kusikilizwa kwa muda mahakamani hapo kutokana na wakili wa Wema kutokuwepo mahakamani hapo, ambapo imeanza kusikilizwa majira ya saa 6:30, leo mchana.

Wema na wenzake wanashtakiwa kwa kosa la kukutwa na kutumia bangi ambapo kesi hiyo itaendelea tena Agosti 4, 2017.

Na Denis Mtima/GPL

KUPATA HABARI NA MAISHA YA UGHAIBUNI BONYEZA HAPA CHINI ;KWENYE YOUTUBE CHANNEL YETU USISAHAU KUSUBSCRIBE