Kutana na msanii Frank Salumu , muigizaji huyu ametokea congo ila anaishi denmark ni msanii ambaye nyota yake imengarakuanzia mwaka 2011 mpaka sasa bado ameweza kukaa juu kwenye kazi zake za film na kumfanya akubalike nchini denmark na nchi mbalimbali za ulaya na hizi ni baadhi ya movies zilizomtambulisha msanii huyu Dont look down to the poor, if i knew. Pasport Love. Ahadi ,Moyo Wangu na nyingine nyingi … pata mawili matatu kutoka kwake.
HABARI YAKO
salama kabisa , nashukuru
HONGERA SANA KWA KUWEZA KUKAKA JUU TOKA 2011 MPAKA SASA,TUPE SIRI YA MAFANIKIO
asante sana , siri ni kujituma , kufanya kazi kwa malengo na siku zote Mungu anakubaliki tu.
Frank Salum na Ashley toto wakishuti Moyo Wangu Film
CHANGAMOTO GANI UNAPITIAKWENYE KAZI YAKO
Mimi siku zote ni mtu wa kazi , ila kukariri script ndio changamoto yangu kubwa , hahahahahah lakini siku zinavyozidi kwenda navyofanya kazi zaidi , nazidi kuwa mwepesi na nawaahidi mashabiki wakae mkao wa kula , frank atakuja na mambo mapya, mwaka mpya mambo mapya wajiandae .
Frank Salum akiwa location akifanya mambo yake
NINI MIPANGO YAKO YA BAADAE
Mipango yangu ni kuendelea kufanya kazi nzuri daima zitakazofundisha , kuelimisha na kuburudisha , kusonga mbele zaidi na kundi langu.
Swahili movies inashukuru sana Frank sakum kwa ushirikiano wako.. tunakutakia kazi njema
Usisahau kulike and share pia unatupata facebook . swahili movies .com
pia follow us instagram swahilimovies