Lucy Komba Adaiwa Kumchana Ashley Toto Redioni Mwenyewe Lucy Afunguka.

LUCYF.K.PIC071Lucy komba

Lucy Komba Hivi karibuni Star mkubwa wa filamu za Swahiliwood Lucy Komba alidaiwa kumnanga muigizaji chipukizi toka Kenya anayeishi Ujerumani Ashley Toto wakati akifanyiwa interview na Swahili talk radio ya nchini Denmark. Chanzo kimoja kikizungumza na SwahiliworldplanetLucy kafanya Interview na radio moja hapa Europe… So kaongea kama vile anamchukia au ana beef flani hivi na Ashley Toto, kasema eti amekuja Europe na akaambiwa kuna mastaa now hapa Europe na wana majina makubwa…akataka kuona hiyo movie aloigiza Ashley, alipoona akasema hakuna kazi yoyote hapa ni kelele tu kapiga na scandals nyingi wala hana lolote…. So watu wengi wameanza kumuuliza Ashley kama ana beef na Lucy ila hajaongea kitu”


Baada ya kuzipata habari hizo ilibidi kumsaka lucy lakini hakuwa hewani kwa muda huo kwa hiyo ilibidi kumsaka msanii mwingine ambaye alihusika pia katika interview hiyo na kuulizwa kama Lucy alimtemea nyongo Ashley au lah jibu lake lilikuwa “Sio kweli kabisa Lucy hajamponda Ashley Toto wala hata kumtaja kwa jina au kwa namna yoyote ile….sio kweli kabisa” alisisitiza msanii huyo

1947659_10202710494511075_1059320109_nAshley Toto

Hata hivyo baadaye Lucy akawa hewani na alipoelezwa kuhusu kumchana radioni Ashley Toto star huyo wa muda mrefu na mwenye uwezo wa kuuva uhusika katika filamu alisema”ha ha ha sijamponda nani kakwambia yeye mwenyewe? sijampoda ila aliniuliza niwashauri nini wasanii wa huku nikamwambia wafanye kazi siyo mtu anacheza scene moja anaanza kujitangazia ustar watu wanatakiwa waone nini msanii kafanya ndiyo wampe sifa hiyo ndo kazi ya sanaa lakini sijaponda yeyote wala sijataja jina la yeyote mbona wasanii wa hivyo wako wengi lakini nashangaa watu wanapenda umaarufu au wanapenda ugombana au kujibizana na mastar ili wawe mastar kupitia sisi kuna mwingine nae analalamika eti mimi nimemponda siyo huyo tu wanajoshtukia na kama wanahizo tabia kweli waache”

Lucy ambaye anasifika nchini Tanzania kwa kujipatia umaarufu kutokana na filamu zake na sio skendo kama baadhi ya mastaa wenzake walivyo alisema kuwa hata hamjui huyo Ashley “Ila huyo msanii mimi simjui wala sijawahi kuona kazi alizocheza na pia waache kujitangazia u-star.  U-star unakuja wenyewe taratibu siyo wa kujilazimisha aache kelele afanye kazi watu waone, mastar wenyewe wamekaa kimya”

Star huyo wa filamu za Yolanda na Pretty Teacher alimalizia kwa kusema ” halafu kawaida yangu huwa sipendi mabifu na watu ndo maana huwa nakaa kimya ila wakinichokoza nitaongea, ila watu wanataka nicharuke maana kila ninachofanya wanaanza maneno nikicharuka hawatanishika waambie. huwa sipendi upumbavu…..waandikie ninachoongea. nimefunga mdomo.kwa muda mrefu ila mbwa ukimzoea anakufuata mpaka msikitini sasa sitaki mazoea na mbwa”

CREDIT :    swahiliworldplanet

Follow us on instagram swahili movies and Like our facebook pages Swahili movies.com and  for more updates about Swahili movies latest news, Scandal, Celebrities, features,european news, American,Australian ,Africa news, Music , news and more