Matusi ya kwenye mitandao ya kijamii yamuumiza Wema Sepetu kwa kumgusa mama yake Mzazi

 

wema7

Wema na Mama yake

Mtandao maarufu wa kijamii wa Instagram umekuwa sehemu ambayo mambo mengi yanafanyika siku hizi na kuwaacha watu wengine wakifurahi, kukasirika na wengine wakitoa machozi kutokana na vita isiyo rasmi inayoendeshwa na team zinazoundwa na mashabiki wanaodai kumlinda mtu fulani maarufu.

Vita ya “team” hizi imekuwa serious zaidi kwa wasanii wa kike na mara nyingi hushambuliana kwa maneno na hata matusi ya nguoni pale mmoja anapotaka kuvuka msitari wa mwingine.

Vita hiyo imemgusa Wema Sepetu na kumuumiza zaidi baada ya kuvuka na kumgusa mama yake mzazi kwa matusi waliyokuwa wakimmiminia Wema.

Kupitia Instagram, Wema ameeleza jinsi alivyoumizwa na matusi  hayo hasa kwa kumuingiza mama yake asiye na hatia katika ugomvi wao.

“Dah…! Sijui hata niseme nini…! Ila si mlitaka kuniumiza… leo mmefanikiwa… nawapeni hongera…. Tena mmetisha haswa… Kila sjku huwa hata siumizwi na matusi yenu cuz naonaga kama ni mnajisumbua tu… Hakuna siku nimelia kwa uchungu kama leo… I min mnitukane mimi mpaka mchoke but leave my mum out of it… Kawakosea nini nyinyi mama angu mpaka mfanye hivyo… Mzazi nwenyewe ndo nimebakia nae mmoja tu… mnataka afe na yeye nibaki yatima sio… dah… leo mmeniweza… saana jamani… Basi naomba isifike huko… nina uchungu sana na mama angu … nampenda sana mama angu ila naona mnataka kuniulia mama angu… Picha halisi ndo hio hapo juu kweli mtu uende ukamfanyie hivyo mama wa mwenzako… una mama wewe.. au uliokotwa na hujui uchungu wa mama… dah… nime surrender leo…. hongera zenu narudia tena… mmeniweza leo…. dah… Mungu nipe nguvu ktk hili jamani… Kwani nilichokikosea haswa ni kitu gani mpaka iwe hivi . Nimekosa nini mimi yarabi toba…. Eeeh mungu… Dah… Ila nashkuru…..”

Nini maoni yako kuhusu mambo kama haya ya uzalilishanaji kwenye mitandao ya kijamii?

Follow us on instagram swahili movies and Like our facebook pages Swahili movies.com and  for more updates about Swahili movies latest news, Scandal, Celebrities, features,european news, American,Australian ,Africa news, Music , news and more

CREDIT :Bongo movies

Tupe maoni yako hapo Chini..!!