Baada ya ukimya mrefu Abou Twaleb aongea Mazito kwa wasanii wa Ulaya soma hapa

1491329_390558261089385_838402233_oActor  and producer Abou  Hermis Twaleb

SM: NI KIMYA KIREFU ABOU HUJASIKIKA TOKA TULIPOONA TRAILER

Ni kweli  nimekuwa kimya kwa mda mrefu nilikuwa bize nikishughulikia mambo yangu ya kazi laki  kuongelea kuusu  wasanii walioingia sasa kwenye gemu au walio na ndoto ya kuingia kwenye tasnia ya Film. Kutokana na tofauti fofauti nyingi zinazoonekama kwa wasanii hawa, zikiwemo…kuchukiana, kuoneana wizu, kurudishana nyuma, kukatishana tamaa na mambo mengineyo kama hayo, kuwa umuhimu mkubwa sana wa kuwakumbusha wasanii chipukizi kuwa maendeleo na mafanikio yatategemeana na nguvu zao wenyewe kabla ya kuwakaribisha wasanii wakubwa ili wawainue. Kumekuwa na tabia sisi kama wasanii

 

1551681_422957367849474_1408049178_n Producer Abou  Hermis Twaleb akiwa editing

wapya kuwategemea sana wasanii wakubwa kimaendeleo na hata kiushauri…hilo nalikubali na naliheshimu sana, ila kwa wasanii tunaoishi EUROPE au ulaya kwa ujumla tuna nafasi nyingi sana za kujiendeleza na kujitangaza zaidi ya tunavyofikiria sisi, Mfano mzuri ni huu: Sisi wasanii tuliobahatika kuishi Ulaya milango iko wazi na ni bure..kimasomo, lna hata kimaisha ukilinganisha na wenzetu waliopo tulipotoka “AFRICA”. Wasanii waliopo Africa kwa mfano TANZANIA ambapo wamepiga sana hatua kwa kiwango cha juu sana, wengi wao wanatamani sana wapape nafasi ya kuishi Ulaya ili waendeleze vipaji vyao…wengine nafasi ni ngumu sana kuzipata au hata connection hawana, lakini sisi ambao tupo tayari EUROPE kwa nini tusiamke na kutumia fursa na kila bahati tuliyonayo ili tujiendeleze kiusanii na kielimu kwa kuwa ni bure. KWA NINI ISIFIKIE KIPINDI IKAWA WASANII WAKUBWA WALIOPO AFRICA WATUKIMBILIE SISI TULIO UPANDE WA NAFASI ZADI…??

Kuna wasanii tunaowaita “STAR AU SUPER STAR” tunaweza kuwaheshimu sana kwa mchango wao mkubwa katika swala zima la kukuza na kuendeleza fani, lakini tukubali kuwa sio kila STAR AU SUPER STAR atapenda kukuongoza kama ndoto zako wewe zilivyo…ikiwa wewe unanafasi zaidi ya kujiongoza, tumia uwezo wako na nafasi uliyonayo ili usonge mbele kiusanii na usingoje tu kuinuliwa…ukweli ni kwamba hata wasanii wakubwa nao huvutiwa na wasanii wadogo na ndio maana hupenda kufanya nao kazi.

1458715_392684520876759_15882465_n

Tujiulize maswali kama haya: kuna msanii gani Africa asiyependa kuhamia na kufanya kazi EUROPE .??? jee kuna wasanii wangapi wasiopenda EUROPE na wanataka kurudi AFRICA ??? Je kwa nini hata tunapofanya Filam zetu tunajiuliza tutauza wapi ??? au kwa nini kila kwenye filam zetu ni lazima tukae na tufikirie ni Msanii gani mkubwa tumshirikishe ili tuweze kuuza kazi zetu ???…..naelewa ugumu wa soko la hapa Ulaya, ila tukumbuke hata kule AFRICA au TANZANIA walipoanza kusambaza kazi zao soko lilikuwa GUMU SANA, nakumbuka sana kwa kuwa Mimi nilikuwa mmoja kati ya Designers wakubwa wa Covers za kazi zao..walikuwa wakijituma sana ..lakini mapato ni kidogo sana. leo hii wameendelea na wanazidi kudai haki zao zaidi na naamini watafanikiwa. JE SISI TUNATEGEMEA NINI HATMA YA KAZI ZETU EUROPE ???

 Naomba tuinuke na tujiulize tuko kweli EUROPE ?? na tuko tayari kweli kuendelea kubaki kama tulivyo ??? Huu ni wakati muafaka wa kupigania katika kujitangaza , kujielimisha, kujiamini kwa kupunguza mawazo ya kuwa bila masanii wakubwa kutuonyesha njia hattaendelea..HIZO NI NDOTO POTOFU…kila kikundi hapa scandinaian hata Holland na europe nzima kwa ujumla kuna wasanii wazuri sana na wenye uwezo wa hali ya juu…tutumie fursa hii ili wenzetu nao watukimbilie , badala ya sisi kuwakimbilia wao. Twaleb Entertainment inawatakia wasanii wote wa vikundi vyote kila la kheri katika kujiinua na kubadilisha mbili za kimaendeleo badala ya kukaa na kusubiri wasanii kutoka nje ya nchi , au kutoka AFRICA ili waje watusaidie…

Follow us on instagram swahili movies and Like our facebook pages Swahili movies.com and  for more updates about Swahili movies latest news, Scandal, Celebrities, features,european news, American,Australian ,Africa news, Music , news and more