MWANAMKE AUAWA SOMALIA KWA KUTOVAA HIJAB

 

1620423_469318463205621_6203797905550909781_n

MWANAMKE AUAWA SOMALIA KWA KUTOVAA HIJAB
Watu wenye silaha nchini Somalia wamempiga risasi na kumuua mwanamke mmoja Muislam kwa kukataa kuvaa hijab, wamesema ndugu zake.
Ruqiya Farah Yarow aliuawa nje ya nyumba yake karibu na mji wa Hosingow, na watu wenye silaha kutoka al-Shabab, wamesema ndugu wa mwanamke huyo.
Watu hao walimtaka avae hijab, wakaondoka, na waliporudi na kukuta hajafanya hivyo wakamuua, wameongeza kusema ndugu hao.
Hata hivyo msemaji wa al-Shabab amekanusha kuhusika na mauaji hayo.
Al-Shabab haidhibiti eneo hilo kikamilifu amesema.
Alipigwa risasi mara mbili na kufa papo hapo. Ameacha mume na watoto. Mwandishi wa BBC anasema kutokana na al-Shabab kukanusha kuhusika na mauaji hayo inaonesha kuna kundi ndani ya kundi hilo waliotekeleza mauaji hayo.
Amesema inawezekana pia al-Shabab wanajiweka mbali na tukio hilo kwa kuwa huenda likaleta ghadhabu kutoka kwa wananchi.

Follow us on instagram swahili movies and Like our facebook pages Swahili movies.com and  for more updates about Swahili movies latest news, Scandal, Celebrities, features,european news, American,Australian ,Africa news, Music , news and more

CREDIT :BBC

Tupe maoni yako hapo Chini..!!