Mzazi mwenzie Alikiba afunguka kuhusu matunzo ya mtoto wao

Baada ya kusambaa tetesi kupitia mitandao ya kijamii kuwa msanii Alikiba ni kati ya wasanii ambao hawatunzi watoto wake moja ya mwanamke ambaye amezaa naye mtoto wa kiume Mama Unju amefunguka na kuweka wazi juu ya sakata hilo.

Mama Unju amesema kuwa mwanamke ambaye amezusha jambo hilo ni muongo bali amekuwa akijitahidi na kupigana ili kuweza kurudisha penzi lake kwa msanii huyo Alikiba hivyo baada ya mambo kuona yanakwenda ndivyo sivyo ndiyo maana amezusha hilo kama njia ya kutaka kumchafua msanii huyo.

Aidha Mama Unju amekwenda mbali zaidi na kutoa ushauri kwa wanawake hao ambao wamezaa na Alikiba na kuwataka kutotumia watoto wao kurudisha mapenzi kwa Alikiba au kutumia watoto wao hao ili waweze kusaidiwa ukoo mzima bali kila mmoja akomae na kupamba na hali yake kama ambavyo yeye alikubaliana na hali baada ya wao kutengana.

Mbali na hilo mzazi mwenzie na Alikiba alimpa ushauri Alikiba na wanaume wengine kuwa wanatakiwa kuangalia aina ya wanawake ambao wanaamua kuwa nao kwenye mahusiano kwani si kila mtu anaweza kuwa na nia nzuri na kuwa wapo watu wengine hawajielewi na hawajui kile wakifanyacho.

XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX