Tuambie historia yako ya Maisha na kipaji chako cha Muziki kwa Urefu
Watu wana niita KAKA COOL Byams ,Jina lenye mama yangu ali nipa ni Byaunda Mchimbwa linalo maanisha Apendavyo Mungu ndivyo afanyavyo.(mapenzi ya Mungu)
kaka Cool Byams akiwa kwenye pozi
Mimi ni mwimbaji tena president wa G. A. S Pro inayo maanisha Gospel Production.
yaani kazi ya ku record video clips, movies na Audio music za kuelimisha jamii na pia za ki kristo. nchini Holland
Nime zaliwa ndani ya familia ya kikristo tena yenye inayo fahamu sana kuimba gospel,
ijapo familia yangu tunajua kuimba, hakujawai mtu yeyote kati yetu kusambaza uimbaji
GABY muimbaji pamoja na kaka cool
Kitu gani kilikupelekea kuimba Gospel Music
Niliona kuimba nyimbo za gospel ni mahubiri so nikaona acha ni wape watu angalau maneno fulani ya biblia na jisi tuna weza kujilinda ndani ya dunia hii yenye walimwengu wa baya.
Naweza kusema mimi lakini si mimi tu ninaye ndugu yangu Tunaye saidiana naye na kwa ukweli naye pia ali pewa kipaji cha kumwimbia Jehova. Kwa jina anaitwa Gaby au Mauris, yeye ana panga sauti vizuri sana na kabisa G. A. S Pro ni yake pia.
Hata tukienda kwenye studio mbele ya kuimba uwaga na mwangalia sana na kumuuliza hapa tu teremshe wimbo vipi, utakuta tayari anayo solution, yaani naweza sema yeye ni solutionman ndani ya G. A. S Pro. na hata nyimbo zingine uwa tuna andika naye. Mungu ambariki.
Changamoto gani unakutana Nazo , Watu wanapokea vipi kazi zako
Kusema kweli nabii ana heshima kwao lakini, sababu napendelea zaidi maneno ninayo imba watu waitumie lakini nimeona uwaga wana dharau zaidi na kutazama huyu ni nani anaeimba hivi badala ya kuangalia MUNGU ANASEMA NINI KUPITIA NYIMBO ZETU.
Nyimbo zako Umeshaweka kwenye Internet au watu wanazipata vipi
Sija wai kutia nyimbo zangu kwenye public namaanisha kwenye internet, sababu nilikuwa bado sijawa tayari kwa kuhanza kazi yangu
Nimewai kupiga kwenye uzinduzi wa NGG- Production, na watu wali penda sana iyo ili nipa nguvu zaidi za kusonga mbele na kumshukuru Mungu zaidi. Mungu awa bariki pia
Ila kuanzia leo mpenzi wa gospel, nimekuja na nguvu nyingi za roho mtakatifu kwa ku kufurahisha zaidi sana
Una mpango gani wa kazi zako za baadae
kwenye mziki wa gospel. Nita kuletea albam mpya inayo itwa 100% MAMBO YA MUNGU (100 percent mambo ya Mungu)
na albam iyo bado aija kwisha ila nime kuletea angalao kipande cha concert video ya wimbo wa kwanza unaoitwa Worship :Hakuna Mungu kama wewe na
kipande cha audio cha wimbo unaoitwa Alleluya Amen.
Uki penda kwenye sherehe yako ao kwenye ukumbi wowote ule kupata mziki wa gospel niko tayari ni contact mara moja kwenye:
byaunda@gmail.com, 0644258376 of kwenye facebook: https://www.facebook.com/KAKA.COOL.BYAMS
https://www.youtube.com/watch?v=iAIO5XAG-mQ
Follow us on instagram swahili movies and Like our facebook pages Swahili movies.com and for more updates about Swahili movies latest news, Scandal, Celebrities, features,european news, American,Australian ,Africa news, Music , news and more
CREDIT : Here
Tupe maoni yako hapo Chini..!!