NI NGUMU KUAMINI,, MIAKA MINNE FILAMU 5 TU ZIMEUZWA!

 

Ni takribani miaka minne tu ya tasnia ya filamu ambayo imeweza kuweka takwimu za mauzo kwa filamu ziliouzwa na zinaendelea kuuza hadi leo hii, katika hilo filamu zinazotamba sokoni hadi leo ukitoa kazi za marehemu Steven Kanumba pekee ndiyo anayebeba kundi la mastaa ambao kazi zao zimeweza kutamba na kufanya vizuri, kuna wale
ambao wanaamini kutokana na kifo cha Kanumba hali ya soko imeshuka, linaweza kuwa na ukweli au watazamaji wamekosa kitu cha kutazama katika filamu zetu.

 

20percent_furaha_iko_wapi-532

Historia inaonyesha kuwa filamu za Swahiliwood ndio zilizozitoa sokoni filamu za kigeni, nakutawala jambo kila mpenda maendeleo alifurahia hali hiyo jamii kupenda kazi ambayo wengi tunaamini kuwa ni ngumu
Lakini kila siku zinavyoyoyoma kwa bahati mbaya mauzo yanabaki katika baadhi ya filamu ambazo hazidi 5, kwa haraka haraka utaona toka mwaka 2010 hadi ni filamu moja tu, imeendelea kuuzwa na kuitajika na watu hadi leo ni Furaha iko wapi 20%.

Katika soko kuna changamoto nyingi huku, ikiwa kila msambazaji anapoingia katika biashara hiyo, kupitia katika njia zilizopitiwa na wasambazaji wa awali ambao walifeli, kutumia majina ya watu fulani ambao nao hawaoni umuhimu wa kuwa na hadithi bora.

Si hivyo tu bali hata wanaoshikilia soko hilo kukosa weledi katika masuala ya filamu, ni moja ya mambo yanayochangia sana kushuka kwa soko hilo, lakini changamoto nyingine ni ujio wa stempu za TRA inasemekana baadhi ya wasambazaji hawakuwa tayari kwa ujio wa Stempu hizo.

 

bado_natafuta1-539

Kitaalamu nitaelezea kasoro ya Stempu hizo katika makala zijazo, zimetajwa filamu 5, ni utafiti

uliofanywa na taasisi ya filamu ya Swahilifilm yenye makazi yake Morogoro unayoundwa na wadau wa filamu.

Hizi ndizo baadhi ya ndondoo za matokeo ya utafiti wa soko la filamu za kibongo ambayo naamini wengi wa wanaojiita wadau hawatayafurahia lakini ndiyo hali halisi.

1. Filamu 5 zilizowahi kuuza zaidi katika historia ya soko ni 20% Furaha iko wapi, Mwali wa Kizaramo, Bado Natafuta, Ndoa yangu na Kigodoro. Kati ya hizo, Bado natafuta, mwali wa kizaramo na Kigodoro zinaendelea kuuza sokoni na hazikai madukani.

– Ukiangalia filamu hizi zimeingia sokoni kwa tabia ya kufanana kasoro ya Ndoa yangu ambayo ilichagizwa na kifo cha Kanumba.

Tabia hiyo ni kuwa watu hawakuzinunua pale tu zilipotolewa ila zilianza kuuza sana baada ya wale walionunua kwanza kuwasimulia wenzao

kigodoro-500

(kwa maana waliobaki katika kava ni wasiojulikana).
Inadaiwa kuwa JB naye anaweza kuuza akisimama peke yake lakini hajawahi kujiamini, kutoka na hali hiyo kutojiamini JB amekuwa akibebwa na wasanii hawa Amri Athuman ‘King Majuto’, Shamsa Ford, Gabo na bi. Hindu.

Baada ya kutambua msukumo wa mauzo kwa kuwashirikisha wasanii hao imekuwa kama vile Family mater kila uonapo tangazo la filamu za JB unaweza kupuuzia kwa kudhani tayari ulishaiona kutokana kusikia au kuona wasanii wale wale.

Steven-Kanumba-pics

 

 

 

 

 

Ndoa-yangu-454

Filamu ambazo hazijachuja sokoni ni za marehemu Steven Kanumba, na kadiri siku zinavyoenda ndivyo zinazidi kupata mashabiki.

Hiyo ni sehemu ndogo ya utafiti wa hali ya soko la filamu Swahiliwood au maarufu kama Bongo movie, kama nilivyosema awali ni kwamba filamu zinazotamba na kudumu sokoni si za mastaa maana yake kuwa wasanii chipukizi wanaweza kuwa bidhaa bora kuliko nyota kwa hali ya sasa ya soko inavyoonyesha.

Ushindani wa wasanii wawili katika tasnia ya filamu Swahiliwood yaani namuongelea Ray na Kanumba nao inawezekana ikawa ni sababu ya mtikisiko wa soko la filamu Bongo, swali linakuja je Marehe Kanumba kaondoka na soko la filamu Bongo? Ni swali naomba unisaidie kujibu.

Follow us on instagram swahili movies and Like our facebook pages Swahili movies.com and  for more updates about Swahili movies latest news, Scandal, Celebrities, features,european news, American,Australian ,Africa news, Music , news and more