Ommy Dimpoz Agoma Kuzungumzia Ishu ya Mama Diamond (Video)

Msanii wa muziki Bongo, Ommy Dimpoz amesema hawezi kuzungumzia ishu ya post ya mama mzazi wa Diamond katika ukurasa wake wa Instagram.

“Hayo mengine yanayotokea is just a game lakini siyo vitu vya kushikana mashati au kumwagiana tindikali, hatujafikia huko ila ukiangalia industry zote duniani hayo mambo yapo na vinachagia wanamuziki kuumiza vichwa zaidi,” amesema Dimpoz.

“Tukiongea tunakuwa tunarudisha hayo mambo tena nyuma, mimi mwenyewe sasa hivi hata menejimenti imesema bwana hayo mambo husizungumzie tena. Hayo mambo tukizungumza tutaamsha hisia, inakuwa haijakaa sawa, nafikiri yaliyopita yamepita,” ameongeza.

Ommy Dimpoz ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘Cheche’ aliingia katika vita kali ya maneno mtandaoni mara baada ya kuposti picha akiwa na mama mazazi wa Diamond na kuweka maelezo ambayo yalileta utata mkubwa na kukosolewa vikali, hata hivyo posti hiyo ilikuja kufutwa baada ya muda.