Serikali yaitaka kampuni ya steps kusitisha ushushwaji wa bei za filamu.

 

687474703a2f2f312e62702e626c6f6773706f742e636f6d2f2d355a65617553476743396f2f564b554164506a673575492f4141414141414147367a6f2f4b726f494b4c596b706d772f73313630302f53637265656e25324253686f74253242323031352d30312d30312532426174

Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ya Tanzania  imepokea malalamiko kutoka kwa wasambazaji wa filamu kuhusu ushushwaji wa bei za filamu uliotangazwa na Kampuni ya Steps Entertainment. 

Wizara imeyashughulikia malalamiko hayo na kuona kuwa bei iliyotangazwa na Kampuni ya Steps Entertainment si halisi na itasababisha tasnia ya filamu kudharauliwa  na pia haina tija katika tasnia ya filamu. 

Wizara inaiagiza kampuni ya Steps Entertainment kusitisha kuanza kuuza filamu hizo kwa bei ya Tshs. 1000 mpaka hapo muafaka utakapopatikana katika kikao kitakachofaninya kati ya Wizara ya Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo, Wizara ya Fedha na Wizara ya Viwanda na Biashara. 

IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO.

Follow us on instagram swahili movies and Like our facebook pages Swahili movies.com and  for more updates about Swahili movies latest news, Scandal, Celebrities, features,european news, American,Australian ,Africa news, Music , news and more

CREDIT :Bongo Movies

Tupe maoni yako hapo Chini..!!