Sherehe Za Miaka 50 ya Muungano Wa Tanzania Bara na Visiwani 2014 Kufanyika Berlin

325793_223931631035859_305532615_o

Sherehe Za Miaka 50 ya Muungano Wa Tanzania Bara na Visiwani 2014 Kufanyika Berlin

Habari za leo mabibi na mabwana
ni mategemeo yangu kuwa wote mnaendelea vizuri na shughuli zenu za kila siku. Kilichopo mbele ya macho yetu ni Miaka 50 ya Muungano wa Tanzania Bara na Visiwani. Umoja wa Watanzania Ujerumani (U T U e.V) , Umoja wa Watanzania Berlin Brandenburg, (UWATAB e.V) kushirikiana na Ubalozi wa Tanzania nchini Ujerumani Kuandaa sherehe za miaka 50 ya Muungano wa Tanzania Bara na Visiwani. Sherehe hizo zitafanyika kuanzia siku ya Ijumaa ya Tarehe 25.04.2014 na kumalizika siku ya Jumamosi ya Tarehe 26.04.2014
Kwa niaba ya
Kamati maalum ya maandalizi
Ubalozi wa Tanzania Ujerumani.
Umoja wa Watanzania Ujerumani (U T U e.V)
Umoja wa Watanzania Berlin Brandenburg ( UWATAB e.V)

Tunayo furaha kubwa kuwaalika Watanzania wote wanaoishi hapa ujerumani na wale wanaoishi nje ya ujerumani pamoja na wenyeji wetu hapa ujerumani, Katika sherehe hii kubwa na ya aina yake, ambayo inajenga historia ya Taifa letu la Tanzania.

Mukhtasari wa Ratiba
Siku ya Ijumaa ya Tarehe 25.04.2014
Midahalo: Wahadhri mbali mbali watatoa mada
Wapi: Tutawaarifu baadaye

Siku ya Jumamosi ya Tarehe 26.04.2014
Reception :
Muziki : Muziki, chakula, vinywaji n.k
Wapi: tutawaarifu baadaye

Ili Kujaza Ratiba ya siku mbili hizi Kamati maalum ya Maandalizi ya sherehe hii kubwa, inategemea kuwaalika Wahadhiri kutoka Tanzania, wahadhiri wa hapa ujerumani, na Bendi ya Muziki itakayoburudisha, kutoka Tanzania. Mialiko hii inategemea na nafasi ya waalikwa hao kulingana na Ratiba zao za kazi.
tutawaletea taarifa zaidi kuhusu Ratiba ya sherehe hii kadiri matayarisho yanavyoendelea kukamilika.

Shughuli ni watu na watu wenyewe ndio sisi. Watanzania tunaoishi ujerumani sherehe hii imetusimamia mlangoni kwetu, hivyo tujitokeze kwa wingi ili tuweze kuitangaza nchi yetu, tuweze kufurahia Muungano Wetu, pia kuja kwako utakuwa umechangia mchango mkubwa sana wa kufanikisha sherehe hii muhimu kwa Taifa Letu.

Mawazo, Ushauri, na Maswali tunayapokea sana kwa mikono miwili. Wasilinana na sisi mara unapoona una swali ushauri au mawazo ambayo yataiwezesha sherehe hii kubwa na muhimu kufanikiwa.

Wanaohitaji malazi Berlin Tafadhali wawasiliane nasi mapema iwezekanavyo

Bw. Mfundo Peter Mfundo
Mwenyekiti (UTU e.V)
Mobile +49 (0) 1737363422

Bw. Fulgens Kisalya
Mwenyekiti (UWATAB e.V)
Tel. +49 (0) 306156294