Kutana na Sallai majasiri ni mkongomani mswahili ambaye anaishi Holland ameoa na ana watoto watatu ni mwigizaji lakini pia ni mmiliki wa sallai majasiri Pro. baada ya swahili movies kuona kazi zake za film nzuri anazofanya hasa movie za gospel ndipo ilipoamua kujua machache kuusu huduma yake hii anayotoa ya film na mipango yake tuendelee……
Sallai majasiri
Hongera ulianza lini kazi ya filamu Na nini kilikusukuma?
Mama yangu ni chachu kubwa sana mimi kua na msukumo wa kuigiza ,maana hata yeye nimuigizaji kanisani hata sasa. Tangu nikiwa mdogo niliigiza kanisani kwenye vipindi vya sunday school.
Waooh that is amazing hongeraSasa niambie unaigiza bado kanisani tu au unafanya film pia ?
Vyote na vifanya .kanisani naigiza na film naigiza. Hadi sasa nimesha shiriki filamu tatu ya kwanza kabisa niliigizia Kenya chini ya UNHCR ; Sugar mamy 2010 ya pili niliishirikiana na rafiki zangu hapa Holland UMDHANIAE NDIE KUMBE SIYE na ya tatu ni filamu yangu nilioiandika mwenyewe nikishirikiana na mdogo wangu mpendwa Gilbert . kwa jina la MWANZO WA MWISHO.
Jarno Feenstra , Sandrine , Solange location
Sasa wewe unafanya gospel film na kwenye film kuna vikwazo vingi kuanzia mavazi na uhusika unakabiliana vipi ikiwa wewe umeokoka hasa love scene?
Watu wanapokea vipi swala la wewe au mtu alieokoka kufanya film kwa ujumla
Wengi kwa sasa maana ndiyo mwanzo , wanakutia moyo kisha wanakuvunja moyo wengine wanadhani tu unacheza mchezo wa muda tu . wengine wanasimama na sisi kwa hali na mali. Kazi zinapokelewa tofauti taofauti , shetani anafanya kazi kwa hali ya juu kwa sasa , ndiyo maana kazi kama za injili zinaweza kuonekana kama tu kupoteza wakati. shetani anapambana lakini MUNGU anashinda !!!
Sallai ,Gilbert na Jarno Feenstra wakiwa location
Ila nafarijika sana maana napokea simu na ujumbe wa email kutoka maeneo mbali mbali ya dunia , kunipongeza nakunitia moyo kwa filamu ya MWANZO WA MWISHO haswa watu wazima wanafurahia sana , maana ni filamu unazoweka kuangalia ukiwa na familia nzima , bila kupatwa na aibu ya kuona yanayoendelea katika filamu hiyo
kwa sasa kuna kazi yoyote inakuja au Bado mwanzo na mwisho na itatoka lini Watu wakae mkao wa kula
bado ni mapema sana kusema hilo , lakini movie yangu ya MWANZO MWISHO itapatikana Youtube , kama nilivyo ahidi. Najiandaa sasa kuja na filamu mpya itakayo leta na kufungua ukurasa mpya wa filamu hapa Ulaya na kote kwa ujumla JIPU KANISANI. nitakayo shirikiana na watu ninaowaeshimu na kupenda kazi zao kama , Devotha Alferd , Selembe Toko , Gilbert Fataki , Ashley Toto, Joy Simgala , Rosette Sallai , Esther Fataki ,Jarno Feenstra , Blandine Wakengo , Antoinette K, Guilaine. Majina ni mengi mno nikiyataja na wote ni wenye vipaji na wasio bahatisha…
Una mipango gani ya baadae ,watu wategemee nini ?
Ni vibaya sana kutangaza mipango ya baadae maana kama ukiwa vitani , adui ni ibilisi , Lakini kwa uweza wa MUNGU muumba watu wakubwa kwa watoto wafurahie maana kila ,Mungu atakapo nijalia kutoa filamu , itawabadilisha maishani mwao , haitowaacha kubaki kama awali , watarajie Mungu kusema nao kupitia mimi na wote ninaoshirikiana nao , akiwamo mke wangu , na kaka yangu Gilbert pamoja na marafiki na wapendwa wengi.
Nimepata tena nafasi ya kwenda kushiriki filamu ya UN hapa hapa Ulaya .na Napenda kuwashukuru wote walioziacha shughuli zao na kuja kuniunga mkono ku hakikisha filamu ya Mwanzo wa mwisho inasimama Sandrine Rugohe , Blandine Wakengo Antoinette Rossi,Solange Jacqueline , na Betty Zelalem , Sandrine Prince ,Jarno Feenstra, Gabby Kihota ,Solange Nyarwka ,Director Kate , Gilbert Fataki na wengine ambao labda sijawataja maana niwengi mno . MUCH LOVE
Swahili movies inashukuru sana Sallai majasiri kwa ushirikiano wako.tunakutakia kazi njema
Usisahau kulike and share pia unatupata facebook . swahili movies .com
pia follow us instagram swahilimovies