SIRI NZITO: BIFU LA UWOYA, BATULI & WEMA , sekretari wa wema amchamba irene uwoya hajui kiingereza


Mara baada ya Wema kutwaa tuzo hiyo, kulianza minong’ono ukumbini humo kuwa alipendelewa kabla ya Uwoya na Batuli ‘kununua’ ugomvi huo huku nyuma kukiwa na visa vingine.

NEEMA AFUKUA MAKABURI

Kufuatia sakata hilo, meneja wa Wema, Neema Ndepanya ( Pichani) aliibuka na kumwanika Uwoya ‘laivu’ akisema kuwa amekuwa akimuonea wivu Wema wakati siyo saizi yake.

‘MAUMIVU YAKIZIDI…’

Maneno ya Neema yalikuja baada ya Uwoya kuweka ‘kijembe’ kwenye ukurasa wake wa Instagram bila kumtaja mhusika huku akimwambia mhusika ‘maumivu yakizidi amuone daktari’.

MAKABURI YAFUKULIWA

Kufuatia vijembe hivyo vya Uwoya ndipo Neema alipoamua kufukua makaburi kwa kumwambia: “Sarafu Queen (Malkia wa Sarafu), maumivu yameshazidi, tumemuona daktari na dozi tumeipata na tunaileta kwako kama ifuatavyo Wengi wanaijua Sarafu Series (Tamthiliya ya Sarafu) inayoruka DSTV, series hiyo ilisababishwa na Wema na iliandikwa na mimi hapa na demo yake ikachezwa na Wema…
“Wema siyo saizi yako na dau la Wema lilikuwa kubwa sana na ndiyo maana waliamua kukufuata wewe hapo kutokana na bajeti yao kubana, ikabidi wakufuate wewe …

“Hivi wakati wanamfuata Wema hawakukuona wewe? Sanaa yako ya kutoa macho kama umebanwa na gari la budege

NEEMA BADO…
Neema aliendelea kusema kuwa, nafasi za Wema nyingi huwa anacheza Uwoya kutokana na kuwa Wema amekuwa akikataa kulipwa fedha kiduchu.

HE! UWOYA HAJUI KINGEREZA?
Hata hivyo, Neema alimwambia Uwoya kuwa, amekuwa akijifanya anajua Kingereza, kumbe hakuna kitu na wala hawezi sanaa ya kujipambanisha na Wema.

Mwanamama huyo ambaye ni prodyuza na mwandishi wa miswada wa Bongo Movies alimshauri Uwoya kwamba, inabidi ajifunze kusifia kazi za wenzake ili aweze kusonga mbele na siyo kuwa na chuki na mafanikio ya wengine.
Neema aliendelea kumpaka matope Uwoya huku akimpachika madai mazito yasiyoweza kuthibitika ya ukahaba ambayo yaliibua gumzo huku baadhi ya watu wenye busara zao wakisema kuwa, Neema amevuka mipaka na kama kuna anachokitafuta, atakipata.

“Hajamtaja jina lakini kwa alivyoandika inaonekana wazi maneno yale ni ya Uwoya, sasa hata kama ni ugomvi, si kwa kumtolea mwenzake lugha chafu kama hiyo. Yeye alijuaje kuwa anajiuza? Au huwa wanaenda wote? Hizo siyo skendo za kumpachika mwenzako kwa kuwa hata akitakiwa athibitishe, hana ushahidi,” alisema mama Sakina wa Sinza jijini Dar aliyedai kufuatilia kwa karibu sakata la mastaa hao.

BATULI MALKIA WA UONGO?

Katika kuendelea kupaka wote waliowakosoa majaji waliompa tuzo hiyo Wema, Neema alimpachika Batuli jina la Malkia wa Uongo na kuahidi kumpa kipande cha kuigiza ambacho atavaa uhusika wa umalikia wa uwongo.
SIRI NYUMA YA PAZIA

Katika sakata hilo lililoshika kasi kwenye mitandao ya kijamii wiki hii, uchunguzi wa Ijumaa ulibaini kuwa, nyuma ya pazia kuna siri nzito inayowagusa wahusika hao na siyo ishu ya tuzo ya Wema.

WEMA vs UWOYA, DIAMOND ATAJWA

Kwa muda mrefu, Wema na Uwoya wamekuwa hawapikiki kwenye chungu kimoja kufuatia skendo ya kuporana mabwana akiwemo staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
Uchunguzi huo ulibaini kwamba, wakati Wema akitibuana na Diamond kwa mara ya kwanza kwenye penzi lao, alishtuka kusikia Uwoya akidaiwa kutoka na msanii huyo wakati alikuwa akimponda na kumwita majina ya kumdhalilisha.


YUMO SALAH

Kama hiyo haitoshi, yapo madai kuwa, kuna mtu mmoja jijini Dar maarufu kwa jina la Salah ambaye aliwahi kudaiwa kutoka na Wema na muda mfupi baadaye, Uwoya alichora tatuu ya jamaa huyo baada ya kuingia kwenye mapenzi, jambo ambalo lilizidi kuchochea kuni kwenye moto wa bifu lao.
Mara kadhaa Uwoya amekuwa akikaririwa akisema kuwa hana ukaribu na Wema kwa kuwa si rafiki yake.

WEMA vs BATULI, CHUKI YATAJWA

Kwa upande wa ugomvi wa Wema na Batuli, uchunguzi ulibaini kwamba, wawili hao hawakuanza ‘matatizo’ yao leo kwani huko nyuma walishatibuana mara nyingi.

Hali ilikuwa mbaya zaidi Wema alipohama Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kwenda Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambapo Batuli alijitokeza hadharani na kumtolea mwenzake povu lililodaiwa kuwa na sababu ya chuki nyuma yake.

NEEMA ATAFUTWA

Baada ya kunasa ubuyu wote huo, Ijumaa lilimsaka Neema kujua mengi zaidi kuhusiana na povu hilo alilolitoa na linaloendelea kusambaa kama povu la sabuni kati yake na Uwoya ambapo alifunguka;
“Kama anajihisi ni yeye sawa lakini sikumtaja yeye! Kwanza kwenye hiyo series ya Sarafu wapo waigizaji wengi tu kwa nini ajishuku yeye! Hebu aniache sina mazoea naye na wala sijawahi kuwa rafiki yake mitandaoni.”

BATULI AUCHUNA

Ijumaa pia lilimgeukia Batuli kuweka mzani sawa juu ya kinachoendelea ambapo alipokea simu na kusikiliza madai yote kisha akakata simu.

UWOYA ASAKWA
Jitihada za kumtafuta Uwoya zilifanyika na alipopatikana kwanza alisomewa madai yake ya kuwa na bifu na Wema ambapo alisikiliza kwa muda akakata simu.
Alipopigiwa kwa mara ya pili hakupokea, akatumiwa waraka mrefu juu ya anachokisema Neema katika series ya Sarafu napo ikaonesha kupokelewa na baada ya muda akajibu kwa kifupi; “Atafutwe Isike (direkta wa Sarafu).” Hata hivyo, Isike hakuwa akipatikana kwenye simu.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxhttps://www.youtube.com/watch?v=9oOsRdoEuNM&t=20s