“SIWEZI KUINGIA MAPENZINI NA MSANII WA BONGO MOVIES..WENGI WAPO KIMASLAHI ZAIDI”…MBOTO

Muigizaji wa filamu za Kiswahili, Haji Salum aka Mboto amesema kuwa hawezi kuanzisha uhusiano wa mapenzi na wasanii wa Bongo Movie kwa kuwa anaogopa kuchafuliwa jina na kuumizwa kimapenzi.

1397320_221759601317850_2000107740_o

 

Mboto alifunguka kupitia mahojiano maalum na Zourha Malisa, ambapo amedai kuwa wasanii wengi wa kike wa filamu za kitanzania (Bongo Movies) hawana mapenzi ya kweli na kwamba wengi wanaangalia maslahi zaidi.

554332_101376463356165_597020705_n

Hata hivyo, alieleza kuwa hatamani kuwa na uhusiano na baadhi ya wasanii hao, bali inamlazimu kuzuia hisia zake ili kuepuka mambo mbalimbali yatakayoyumbisha maisha yake.

1779038_246909062136237_730358701_n

“Unajua mimi pia nina tamani na pengine wao wananitamani ila najizuia na wala sitaki kuruhusu majaribu kwani najua ninachokifanya huku kwenye tasnia yetu tunakijua hivyo ni lazima ujiepushe na mambo mengine.” Alisema Mboto.

Ameeleza kuwa kuna waigizaji wengi wa kike ambao ni rafiki zake wa karibu na wanashirikiana vizuri kwenye kazi.

CREDIT: GUMZO LA JIJI

Follow us on instagram swahili movies and Like our facebook pages Swahili movies.com and  for more updates about Swahili movies latest news, Scandal, Celebrities, features,european news, American,Australian ,Africa news, Music , news and more